WAZIRI MKUU MAJALIWA AKATAA VIWANGO VYA NAULI ZA MABASI YA MWENDO KASI

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es salaam, alipowasili kutoka mkoani Ruvuma alikokuwa kwenye ziara ya kikazi. Kubwa alilosema,  Majaliwa ni kuzikataa nauli zilizopendekezwa za mabasi yaendayo kasi,  Majaliwa aliwaambia waandishi wa habari kuwa, viwango hivyo vya shilingi 1,200 na 1,400 huku wanafunzi wakilipa nusu ya viwango hivyo, ni vikubwa mno kwa Mwananchi wa kawaida na haikuwa lengo la mradi huko Ameitaka Tamisemi na wizara ya uchukuzi kwa kushirikiana na waendeshaji wa mradi huko wakajipange upya na wakishindwa serikali itauendesha mradi huko.
Waziri Mkuu Majaliwa (katikati), akiwa na Waziri wa nchi (TAMISEMI) na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky SADICK.

0 comments: