Rais mstaafu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi akiingia chumba cha mkutano cha Nyerere ndani ya mjengo wa Ubalozi Washington, DC siku ya Ijumaa April 24, 2015 kulikokua na kikao cha Mabalozi wa heshima kilichoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani chini ya Balozi Liberata Mulamula kwa ajili kuongelea maswala mbalimbali zikiwemo changamoto za utalii na uwekezaji nchini Tanzania na jinsi gani ya kukabiliana nazo, mbali na Mabalozi hao wa heshima na marafiki zao wengine waliohudhuruia kikao hicho ambacho kilikua sehemu ya maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano ni wawakilishi wa Taasisi za Diaspora za Kitanzania zinazopigana kusaidia maswala ya uwekezaji na Utalii kwa nchi yao Tanzania. Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi pia aliongozana na mkewe Mama Sitti Mwinyi.
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na mwenyeji wake Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula wakiwemo Mabalozi wa heshima wakisimama kwa ajili ya nyimbo za Taifa za Tanzania na Marekani.
Mhe. Liberata Mulamula Balozi wa Tanzania nchini Marekani akimtambulisha Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwa Mabalozi wa heshima wakiwemo viongozi wa taasisi mbalimbali za Kimarekani zinazotangaza utalii wa Tanzania nchini Marekani na baadae kumkaribisha kuongea nao.
0 comments: