BENJAMINI MKAPA AONGOZA HAFLA YA KUJADILI CHANGAMOTO ZA UCHUMI ,FULSA NA MATARAJIO YA VIONGOZI WA AFRIKA KWA SIKU ZIJAZO.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa Profesa Samuel Wangwe(kulia), akiongea na viongozi mbalimbali mara walipo kutana katika hafla ya marais wastaafu Afrika ,wakiongozwa na Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam leo
 Mjumbe wa Kamati kuu ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Profesa Mwesiga Baregu(kulia) akiongea na viongozi mbalimbali,akiwemo  Waziri mkuu mstaafu na makamu wa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Joseph Sinde Warioba,wa tatu kushoto na waziri mkuu mstaafu Dk. Salim Amhed Salim,(wapili kushoto)

 Balozi Juma Mwapachu (katikati),akiongea na viongozi mbalimbali katika hafla ya baadhi ya marais wastaafu Afrika wakiongozwa na Benjamini Mkapa, Dar es Salaam leo,kujadili changamoto za uchumi,fulsa na matarajio ya viongozi wa Afrika kwa siku zijazo.



Rais Mstaafu Benjamini Mkapa,akiwasili katika hafla ya  kujadili changamoto za uchumi,fulsa na matarajio ya viongozi wa Afrika kwa siku zijazo.

0 comments:

WEMA SEPETU AANIKA UGOMVI WAKE NA MAMAYAKE!

Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akiwa na mama yake.
Na Waandishi Wetu
STAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu ametaja sababu zinazomfanya aingie katika mgogoro na mama yake mzazi, Miriam Sepetu kuwa ni suala la uchumba wake na Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambao alikuwa akiupinga mara kwa mara.
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
Akipiga stori na mapaparazi, Wema alisema kwa muda mrefu alikuwa akitofautiana kauli na mama yake katika suala zima la uhusiano wake na Diamond lakini anamshukuru Mungu amemuelewa na sasa kila kitu kinakwenda sawa.
“Mama nilikuwa nikimsihi sana juu ya uchumba wangu na Diamond lakini sasa tumefikia hatua nzuri namshukuru Mungu amekubali, maana siku hizi nikionana naye ananiuliza vipi mwenzako mzima, anaendeleaje, wakati mwanzoni haikuwa hivyo,” alisema Wema huku akiahidi kumkutanisha Diamond na mama yake. Imeandikwa na Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani

0 comments:

MAMIA WAMZIKA HALIDA, NI YULE ALIYEFARIKI KATIKA SWALA YA IDD

waombelezaji_cb4bd.jpg
Wakazi wa mjini Iringa leo wajitokeza kwa wingi kumzika Halida Ng'anguli katika makaburi ya Makanyagio, ni yule aliyefariki siku ya Iddi el fitri baada ya kuanguka chooni katika uwanja wa samora jana.Waislamu nchini jana wameungana na waislamu wenzao duniani kuswali sala ya Iddi mkoani Iringa lakini kwa bahati mbaya muumini mwenzao Halida Ng'anguli mkazi wa Mwangata C ambaye ni shangazi wa manahabari wa gazeti la majira Iringa Zuhura zuhkeri kufariki dunia baada ya masaa machache toka aanguke chooni uwanja wa Samora.
jeneza_a7075.jpg

kaburi_48751.jpg
waombelezaji_3_b2313.jpg
Wakazi wa mjini Iringa leo wakiwa nyumbani kwa marehemu Halida Ng'anguli Mwangata C. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)

0 comments:

ZAHA ATAMBA KUNG`ARA NA LOUIS VAN GAAL

Re-United: Wilfried Zaha and former Red Devil Nemanja Vidic
Wilfried Zaha na beki wa zamani wa United Nemanja Vidic wakichuana.
NA MPEJA BLOG
WINGA wa Manchester United , Wilfried Zaha amesema anatarajia kuwa mchezaji wa aina aitakayo Louis Van Gaal baada ya msimu uliopita kutoswa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo David Moyes.Zaha alitoshwa na kocha Moyes na kumtoa kwa mkopo katika klabu ya Cardiff mwezi januari kwa madai kuwa nyota huyo ana mitazamo mibaya.Kinda huyo mwenye miaka 21, sasa amepewa nafasi ya kuonesha uwezo wake kwa Van Gaal na katika mechi ambayo Man United ilishinda kwa penati dhidi ya Inter Milan, kocha huyo alimwacha Zaha mpaka kipindi cha pili ili aoneshe ujuzi wake katika mechi yake ya kwanza ya maandalizi ya kabla ya msimu.
Old Trafford lifeline: Zaha was handed a chance to impress against Inter Milan
Zaha alipewa nafasi ya kumuonesha uwezo kocha Van Gaal kwenye mechi dhidi ya Inter Milan.

Van Gaal amemuambia Zaha kuwa anatakiwa kujitahidi kuwa mshambuliaji wa kati ili aingie katika mfumo wake wa 3-5-2 msimu ujao.
Zaha alisema: "Nilikuwa nacheza winga, lakini kama kocha anataka nizoee nafasi nyingine, nitafanya,"
"Sio kwamba mimi naweza winga tu, nitacheza nafasi nyingine".
"Nimesikia anataka kuwapa nafasi wachezaji vijana. Hiki ndicho nilihitaji tangu nimefika hapa. Nataka kuwa mchezaji wa Man United. Natumaini kupata nafasi msimu ujao".
Sir Alex Ferguson alimnunua Zaha januari mwaka 2013 kutokea klabu ya  Crystal Palace

0 comments:

FAHAMU UKWELII KUHUSU UGONJWA WA EBOLA

Ugonjwa wa Ebola unasababishwa na Virusi na ni ugonjwa hatari unaoambukiza haraka binadamu na wanyama mwitu (hayawani) kama kima, sokwe, popo, ndege, mijusi, amfibia, na kadhalika. Ugonjwa huu unaosababishwa na virusi aina ya Ebola Virus ni wa mlipuko.
Japokuwa hakuna mazingira maalum ambamo virusi vya Ebola vinapatikana, lakini wataalamu wanasema virusi hivyo vinapatikana kwa mnyama ambaye anapatikana zaidi barani Afrika.
Mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola umetokea katika nchi nyingi na bado unaendelea kupukutisha maisha ya watu wengi hasa barani Afrika. Matukio ambayo yamethibitishwa kuwepo kwa ugonjwa huo ni katika nchi za Liberia, Sierra Leone, Guinea, Ghana, Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Gabon, Sudan, Ivory Coast, Uganda na kadhalika.

 
Ugonjwa wa Ebola daima unasambaa ndani ya maeneo ya utoaji wa huduma za afya.Hata hivyo, matukio mengine yamekuwa yakitokea nje ya maeneo hayo na hayafahamiki.
Jinsi ugonjwa huo unavyosambaa:
Namna ugonjwa huo ulivyojulikana kwa mara ya kwanza hakuna anayefahamu kwa hakika. Hata hivyo, ugonjwa wa Ebola unaweza kusambazwa kwa njia zifuatazo:
1. Kugusana moja kwa moja na mtu ama mnyama mwenye ugonjwa huo;

2. Kugusana moja kwa moja na damu ama majimaji (mate au mafua) ya mtu mwenye ugonjwa huo katika familia;

3. Kugusa vifaa vya tiba vilivyo na virusi vya ugonjwa huo kama sindano;

4. Kutumia vifaa visivyochemshwa katika hospitali kama sinano;
5. Kula ama kushika vinyesi vya wanyama wenye ugonjwa huo;
6. Kuvuta hewa yenye virusi vya ugonjwa huo katika mazingira ya hospitali;
7. Kutumia nyama ya wanyama walioathirika kama kitoweo;
8. Kutozingatia tahadhari za kitaalam.

Dalili za Ebola:
Mtu au mnyama mpaka aonyeshe dalili za ugonjwa wa Ebola huchukua kati ya siku 2 hadi 21. Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na:
1. Homa kali
2. Kuumwa kichwa

3. Kuharisha

4. Kutapika

5. Maumivu ya kifua
6. Maumivu ya tumbo
7. Mafua
8. Kikohozi
9. Maumivu ya misuli na viungo, hasa kwenye viungio
10. Kuvimba koo
11. Mwili kuwa dhaifu
12. Mfadhaiko
13. Kuchanganyikiwa
14. Macho kuwa mekundu
15. Kuvuja damu kwa ndani na nje

Nani aliye katika hatari?
1. Watu wanaofuga wanyama mwitu ama wanaoishi katika maeneo yenye wanyama mwitu;

2. Watu wanaotegemea wanyama mwitu kama popo kama chakula chao;

3. Watumishi wa vyumba ya kuhifadhia maiti;

4. Watumishi wa afya wanaowahudumia wagonjwa wa Ebola;
5. Watumishi wa afya katika hospitali ambazo hazina mazingira bora na safi;
6. Wanafamilia wa wagonjwa wa Ebola;
7. Watu wanaohudhuria hospitali ambazo hazina mazingira safi na salama;

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa Ebola:
1. Epuka kugusa damu/majimaji ya wanyama ama binadamu walio na ugonjwa wa Ebola au hata maiti za watu waliokufa kwa ugonjwa huo kwa kuzingatia haya:
a) Tunza mazingira safi na salama ya hospitali;

b) Watelekeze wagonjwa wa Ebola;

c) Fukia miili ya waliokufa kwa Ebola kwa usalama;

d) Epuka mazishi ya kienyeji kama kuosha maiti za watu waliokufa kwa Ebola;

2. Watumishi wa afya na wanaowatazama wagonjwa wa Ebola wanatakiwa:
a) Kuvaa kwa usahihi vifaa vya kujikinga na nyuso, mikono na macho,

b) Na majoho maalum daima;

c) Kutumia sindano mara moja na kuziteketeza ama kuzifukia;

d) Epuka kutumia zaidi ya mara moja sindano au kutotumia sindano ambazo hazijachemshwa vyema;
e) Epuka kuosha maiti za watu waliokufa kwa Ebola;
CHANZO : BROTHER DANY BLOG

0 comments:

DIAMOND PLATINUMZ ATUWA DAR ES SALAAM LEO

 Diamond Platinumz, akiwa katika gari la wazi akiimba moja ya nyimbo zake akiwa na wadau wake leo mara alipo wasili wakiwa eneo la Faya.(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa www.ujijirahaa.blogspot.com
Ikifunguka ,funguwa ukurarasa wenye herufi kubwa ( UJIJI RAHAA ).
 Wadau wa  Diamond Platinumz, wakiwa wanakimbia huku wameshika bango lenye picha ya Msanii huyo.
 Mshabiki wa Diamond Platinumz, akiwa amepanda gari lenye namba T327 CYC, kwa nyuma wakati wa mapokezi ya msanii huu Dar es Salaam leo 
Dreva wa Bodaboda akiwa  amewabeba washabiki wa Diamond Platinumz,    wakati wa mapokezi ya msanii huu Dar es Salaam leo
 Mwanamziki wa kizazi kipya ,kupitia bongo Movie,Nasseb Abdul "Diamond Platinumz", akisalimiana na Mashabiki  wake mara alipowasili Nchini jana baada ya kutwaa Tuzo mbili za Afrika music Magazine Awald "AFRIMMA2014" kupitia kipengele cha msani bora wa kiume Afrika Mashariki.
 Mashabiki wakiwa katika Bajaji wakimsalimia  Diamond Platinumz
 Mashabiki wakiwa wanatowa mitindo tofauti mara alipowasili Dar es Salaam leo
 Wanahabari wakiwa kazini mara walipo mpokea  Diamond Platinumz,Dar es Salaam leo

 Diamond Platinumz,akiwaonyesha mashabiki wake mara alipo wasili leo

0 comments:

MTEMVU ATOA MKONO WA IDD WA VYOMBO NA SH. 10,000 KWA VIONGOZI 912 WA MATAWI YA CCM TEMEKE

Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia), akimkabidhi boksi la vyombo na zawadi ya sh. 10,000 mmoja wa viongozi 912 wa matawi wa ya CCM na jumuiya zake wa jimbo hilo, katika hafla ya kutoa mkono wa Idd el Fitr Dar es Salaam jana. Kila mmoja alipata zawadi kama hiyo. Katika boksi hilo kuna vikombe, birika, vijigo, sahani na chupa ya chai. Katikati ni mke wa mbunge huyo, Mariam Mtemvu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mtemvu akimkabidhi Mwenyekiti wa UWT CCM tawi la Mji Mpya Kata ya Buza, Temeke.
Baadhi ya viongozi wakiondoka na vyombo vyao huku wakiwa na sh. 10,000 kibindoni.
Shehena ya vyombo vilivyokuwa vinagawiwa
Sehemu ya umati wa viongozi wa CCM wa matawi waliofika kupata zawadi hizo. Wengi walimpongeza Mtemvu kwa moyo wake wa kujitolea.
Ni furaha tele kwa mama huyo.......
                          Mary wa Yombo Kilakala akifurahia zawadi yake na kitita cha sh. 10,000
Mwenyekiti wa CCM Tawi la Mlimani, Kata ya Kilakala, Temeke, Dar es Salaam, Omar Kichapwi huyoooo na vyombo vyake . ndani ya vyombo hivyo kuna vikombe, birika vijiko na chupa ya chai
Mke wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Mariam Mtemvu akimkabidhi zawadi ya vyombo na sh. 10,000 mmoja wa viongozi wa CCM wa Jimbo hilo.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke,  akimkabidhi vyombo na sh. sh. 10,000 mmoja wa viongozi wa matawi wa CCM wa Jimbo hilo. Zawadi hizo zilitolewa na Mbunge wa Jimbo hilo, Abbas Mtemvu (kulia).
Wakifurahia kupata zawadi hizo.

0 comments:

MTOTO ANUSURIKA KUUAWA MARA BAADA YA KUCHOMWA NA MOTO KWA KUTUMIA MIFUKO YA RAMBO NA MAMA YAKE MZAZI

 Miguu ya mtoto Brayan iliyochomwa na mama yake mzazi.
MTOTO, Brayani Emanuel mwenye umri wa miaka sita, amenusurika kuuawa baada ya mama yake mzazi Rose Mwanisisi Mkazi wa kitongoji cha Chemchem kilichopo eneo la Mbalizi Mbeya vijijini, kujaribu kumchoma moto kwa kutumia mifuko ya manila.Tukio hilo limetokea Julai 16 mwaka huu, ambapo imeelezwa kuwa mama huyo baada ya kurudi nyumbani kwake majira ya jioni hakumkuta mtoto,hivyo aliaanza kumtafuta na alipompata alimfungia ndani na kisha kumchoma  moto kwa kutumia mifuko ya manila.

0 comments:

RAIS BARACK OBAMA ASHIRIKI MKUTANO WA VIJANA WA AFRIKA

Rais wa Marekani ,Barack Obama akizungumza na Viongozi vijana toka nchi mbalimbali za Afrika waliokuwa wakipata mafunzo katika vyuo vikuu vya Arkansas na Florida.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry akitoa hotuba yake kwa Viongozi vijana toka barani Afrika waliokuwa wakishiriki mafunzo katika vyuo vikuu vya Arkansas na Florida nchini Marekani.
Rais Obama akiondoka Ukumbini mara baada ya kuzungumza na Viongozi vijana toka nchi mbalimbali za Afrika waliokuwa wakipata mafunzo katika vyuo vikuu vya Arkansas na Florida.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari ni miongoni mwa Vongozi vijana toka barani Afrika waliohudhuria mkutano huo na Rais Barack Obama .
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari ni miongoni mwa Vongozi vijana toka barani Afrika waliohudhuria mkutano huo na Rais Barack Obama hapa akifuatilia kwa makini Hotuba ya Rais Obama. .
Mbunge Joshua Nassari akiwa na Viongozi vijana wenzake walioshiriki mafunzo hayo nchini Marekani.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari  akionesha cheti chake cha kuhitimu mafunzo ya wiki tisa yaliyoshirikisha  Vongozi vijana toka barani Afrika .
Cheti cha kuhitimu Mafunzo ya wiki tisa alichotunukiwa Mbunge Joshua Nassari baada ya kuhitimu mafunzo ya wiki tisa yaliyoshirikisha Viongozi Vijana  nchini Marekani.

 
Ukumbi wa Regency Ballroom katika Hotel ya Omni Shoreham Washington DC ukiwa umepambwa kwa Bendera toka mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania.

0 comments: