Wamenaswa: Mashabiki wawili waliojipaka rangi nyeusi wakiwa katika pozi kwenye mchezo baina ya Ujerumani na Ghana.
Imechapishwa Juni 23, 2014 saa 10:07 jioni
SHIRIKISHO
la soka Duniani, FIFA linachunguza picha zilizozagaa zikiwaonesha
mashabiki wakiwa wamejipaka rangi nyeusi katika mchezo wa kundi G baina
ya Ujerumani na Ghana.
Picha
zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha wanaume wawili,
wanaoonekana kuwa mashabiki wa Ujerumani, wakiwa na sura nyeusi kwenye
uwanja wa Fortaleza jumamosi iliyopita.
FIFA imesema kamati yake ya maadili ipo katika majadiliano ya kufungua kesi.
Chini ya uchunguzi: FIFA inachunguza ripoti zinazoeleza kuwa mashabiki wa Ujerumani walijipaka rangi nyeusi.
Wanatazama mechi: Mashabiki wawili walinaswa na kamera katika sare ya 2-2 baina ya Ujerumani dhidi ya Ghana.
"Siku zote tunachukua ushahidi wote na
kuupeleka kamati ya maadili. Ni kamati ya maadili itakayokutana,"
Msemaji wa FIFA amewaambia The Guardian. "Kama kutaonekana kuna ukweli
kesi itafunguliwa. Hilo lipo juu ya kamati ya maadili, wao ndio
watachukua maamuzi".
FIFA huwa wanayawajibisha mashirikisho ambayo mashabiki wake wanaonesha utovu wa nidhamu uwanjani.
Katika tukio la pili, mtu aliingia uwanjani kipindi cha pili wakati wa sare ya 2-2.
Mtu huyo ambaye hakuwa na shati aliripotiwa kuwa ni Mpoland na alijiandika namba za simu na anwani ya barua pepe tumboni kwake.
Kiungo wa zamani wa Portsmouth na
Sunderland, Sully Muntari, ambaye kwasasa anacheza AC Milan alimsalimia
mtu huyo kabla ya kuondolewa na maaskari wa usalama.
Msemaji wa kamati ya maandilizi ya
Brazil, Saint-Clair Milesi alisema mtu huyo aliingia kutokana na uzembe
wa mamlaka zinazohusika na usalama uwanjani.
Shabiki aliingia uwanjani katika sare ya 2-2 baina ya Ujerumani na Ghana.
0 comments: