Safari ya miaka minne ya mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage inafikia kikomo leo
SIMBA
SC wapo katika mkutano mkuu wa Uchaguzi unaoendelea muda huu katika
Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Uchaguzi
huo unashirikisha jumla ya wagombea 27 ambapo nafasi ya juu kabisa,
Urais, inawaniwa na wagombea wawili Evans Elieza Aveva na Andrew Peter
Tupa.
Nafasi ya Urais inawaniwa na Swedi Mkwabi, Bundala Kabulwa ,
Geofrey Nyange `Kuburu` na Jamhuri Musa Kihwelo `Julio`.
Wanaowania
ujumbe wa kamati ya utendaji ni Said Tulliy, Yasini Mwete, Ally
Suru, Rodney Chiduo, Said Pamba, Ally Chaurembo , Abdulhamid Mshangama
, Chano Almasi, Damian Manembe, Ibrahim Masoud, Kajuna Noor, Hamisi
Mkoma, Alfred Elia na Saidi Kubenea.
Wagombea wengine ni Idd Mkamballah, Juma Mussa, Maulid Abdallah na Collin Frisch. Wagombea.
kwa upande wa wanawake ni Asha Muhaji, Amina Poyo na Jasmine Badour.
Mchakato huu wa uchaguzi umefika hapa ulipo baada ya kugubikwa na mizengwe kadhaa.
Inafahamika kuwa matatizo yalianza siku alipoenguliwa mgombea wa nafasi ya Urais Michael Richard Wambura.
Wambura
alienguliwa na kamati ya uchaguzi ya Simba sc, chini ya mwenyekiti
wake, Wakili Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kwa sababu ya kuipeleka Simba
mahakamani na kusimamishwa uanachama mwaka 2010.
Lakini
`kidume` alikata rufaa katika kamati ya rufani ya uchaguzi ya TFF chini
ya mwenyekiti wake, Jaji Julius Mutabazi Lugaziya.
Kamati
ya jaji Lugaziya alimrejesha Wambura kuendelea na mchakato wa uchaguzi
baada ya kubainika kulikuwa na makosa yaliyofanywa na Simba kwa kumuacha
Wambura aendelee kufanya shughuli za klabu kama mwanachama akiwemo
kulipa ada wakati walimsimamisha.
Lakini
kamati ya Ndumbaro alimuengua kwa mara ya pili kwa sababu ya kupiga
kampeni kabla ya muda. Wambura alikata rufaa tena katika kamati ya
uchaguzi ya TFF, lakini rufani yake ilikataliwa, hivyo kutoka rasmi
kwenye mchakato wa uchaguzi wa Simba sc.
Baada
ya tukio hilo, baadhi ya wanachama wa Simba walienda kufungua kesi
mahakama kuu wakitaka mahakama isimamishe uchaguzi kwasababu Wambura
hakutendewa haki.
Mahakama
Kuu ilikataa kusimamisha uchaguzi huo, na hatimaye leo hii rais mpya,
makamu wa rais na wajumbe wa kamati ya utendaji wanapatikana.
Ilikuwa safari ndefu na wengine waliamini isingetimia, lakini hatimaye kitendawili kimeteguliwa.
Kazi
kwenu wanachama wa Simba. Kwa muda sasa mmesikiliza kampeni za wagombea
wote. Kinachotakiwa ni kutuliza akili kwenye maboksi ya kura ili
wapatikane viongozi sahihi.
Inafahamika
wapo ambao wanaumia kwasababu wagombea wanaowaunga mkono walienguliwa
hususani Wambura, lakini yameshatokea na mwisho wa siku Simba ni yenu na
mnatakiwa kushirikiana kupata viongozi wapya.
Simba inahitaji mabadiliko makubwa, na kwa kuanza, leo ni siku muhimu kwa wanasimba wote.
Zaidi mtandao huu na timu yake unawatakia kila la heri katika uchaguzi wenu unaofanyika leo.
0 comments: