Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa
pili kushoto mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi
wenzake waliohudhuria na kuzungumza katika mkutano huo wa sherehe za
maadhimisho ya miaka 50 ya nchi za G77 na China uliofanyika jana Juni
15, 2014, jijini Santa Cruz, Bolivia. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya nchi za G77 na
China, uliofanyika jijini Santa Cruz, Bolivia jana Juni 15, 2014. Picha na OMR
Sehemu ya washiriki na wawakilishi wa viongozi wa mataifa mbalimbali katika mkutano huo.Picha na OMR
Sehemu ya washiriki na wawakilishi wa viongozi wa mataifa mbalimbali katika mkutano huo.Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
(katikati) akiwa na baadhi ya Viongozi kutoka mataifa mbalimbali wakati
wa ufunguzi wa maadhimisho hayo yaliyofanyika juzi usiku Juni 14,
jijini Santa Cruz, Bolivia. Picha na OMR
…………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Maalum, Santa Cruz, Bolivia
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed
Gharib Bilal amezitaka nchi wanachama wa G77+China, kuhakikisha
zinaboresha kilimo ili ziwe na hifadhi ya kutosha ya chakula kwa wananchi wake.
Akihutubia mkutano wa mwaka kwa nchi za G77+China ambao pia ni
kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya umoja wa nchi hizi, unaofanyika
jijini St Cruz De Sierra, Dkt Bilal alisema nchi za umoja huu zina
maeneo mazuri kwa kilimo na hivyo ni muhimu kuyatumia maeneo haya katika
kuzalisha chakula kwa lengo la kuhifadhi na kuwa na usalama wa chakula
nyakati zote.
Dkt. Bilal alisema, nchi hizi kwa pamoja zinahitaji kuwa na
kauli moja kuhusu masharti yanayowekwa na nchi kubwa hasa katika kilimo
na kuelezea kuwa ili mafaniio makubwa yapatikane, lazima uwepo uwekezaji
wa ndani katika kilimo sambamba na serikali za nchi hizi kuchangia
shughuli za uzalishaji ili kuwa na kilimo chenye tija kwa wakulima na
kinachoweza kuchangia usalama wa chakula.
Kuhusu suala la mazingira,
Mheshimiwa Makamu wa Rais aliwaeleza wajumbe wa G77+China kuwa,
maazimio yaliyofikiwa Rio+20 na mapendekezo kuhusu ‘Kesho tunayoitaka’
yanazihitaji nchi hizi kupaza sauti zake kwa pamoja kuhusu kukabiliana
na mabadiliko ya tabia nchi kwani suala hili kwa sasa haliwezi
kutatuliwa na nchi moja bali linahitaji nguvu ya kila mtu duniani.
Makamu wa Rais alifafanua kuwa bila kuwa na mazingira bora
maendeleo endelevu yatabakia ndoto na pia kufanikisha Malengo ya Milenia
kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa itakuwa vigumu kama suala la
mazingira litaachwa kwa kila nchi kufanya inavyotaka.
“Kundi hili lina kazi kubwa iliyo mbele yetu na hasa kuhusu
malengo mapya ya maendeleo baada ya kukamilika kwa muda wa Malengo ya
Milenia mwakani. Tunahitajika kubuni njia za kuzipatia nchi zetu
maendeleo katika Nyanja za uchumi, kijamii na mazingira ili tufanikiwe vema,” alisema Mheshimiwa Makamu wa Rais.
Katika hotuba hiyo Mheshimiwa Makamu wa Rais pia alizungumzia
kuhusu umuhimu wa nchi hizi kuweka msisitizo wa kuwapa wananchi maji
safi na salama, umuhimu wa kuwa na nishati inayotosheleza matumizi ya
uzalishaji, uwepo wa huduma bora za afya na elimu
ili kupiga hatua kwa haraka baina ya wananchi wa nchi hizi. “Nafahamu
kufanikisha haya yote ni kazi kubwa lakini hatuna muda wa kusubiri. Ni
lazima tufanye kazi ili kubadili hali iliyopo,”alifafanua.
Mkutano huo ambao umekamilika jana kwa mwenyeji wake Rais Evo Morales kuwashukuru wanachama wa G77+China walioweza kushiriki
mkutano huo, pia ulionesha nia kwa wanachama wa nchi hizi kutafuta
majibu ya changamoto ya ukosefu wa ajira unaokabili wananchi wengi wa
nchi hizi. Viongozi wengi walisisitiza kuwa, suala la ajira hasa kwa
vijana linatakiwa kutazamwa upya na hasa ukizingatia rasilimali zilizopo
katika nchi za G77+China ili zitumike katia kutengeneza ajira mpya
zitakazoweeza kusaidia kuboresha maisha ya watu wa nchi hizi kwa miaka
mingi i
0 comments: