Samia amesema vyombo vya habari vikiwa huru vinagusa kila pembe ya jamii kwa kuelemisha , kufichua maovu , kuchangia maendeleo ya kijamii na kukuza demokrasia.
Amesema hayo leo Juni 18,2024 jijini Dar es salaam kwenye kongamano la sekta ya habari na kusema kuwa habari za kiuchambuzi kwenye vyombo vya habari ni chache, hivyo waandishi watilie mkazo kwenye uchambuzi na wajielekeze kwenye habari zinazokubalika
Amesema zama zinabadilika waandishi lazima waendane na mabadiliko yaliyopo ya kiteknolojia na watumie uwezo wao wa taaluma vizuri.
Naye Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amesema Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya habari na Tanzania imekuwa kinara Afrika Mashariki kwa uhuru wa vyombo vya habari.
0 comments: