Rais wa Jamhuri ya Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud akisaini kitabu cha wageni Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Rais wa Jamhuri ya Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud tibabu ya moyo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo na Dkt. Bingwa Magonjwa ya Moyo Dkt. Peter Kisenge.
Rais wa Jamhuri ya Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo na Dkt. Bingwa Magonjwa ya Moyo Dkt. Peter Kisenge. mara alipoitembelea Taasisi hiyo kujionea mtambo wa Cathlab ambao ni maabara inayotumia mionzi maalumu kwaajili ya kufanya uchunguzi na matibabu ya moyo. Wa katikati anae shuhudia ni Waziri wa Afya Nchini Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu wakimo viongozi wengine wa Taasisi hiyo.Rais wa Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud aipongeza JKCI
Na Mwandishi Maalumu - Dar es Salaam
27/4/2024 Rais wa Jamhuri ya Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud amewapongeza wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa huduma nzuri wanayoitoa ya kuokoa maisha ya watu wenye matatizo ya moyo.
Mhe. Rais Hassan Sheikh Mohamud alizitoa pongezi hizo leo jijini Dar es Salaam alipotembelea Taasisi hiyo (JKCI) kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Akiwa katika Taasisi hiyo Mhe. Rais Mahamud alitembelea maeneo mbalimbali ya JKCI ikiwa ni pamoja na mtambo wa Cathlab ambayo ni maabara inayotumia mionzi maalumu kwaajili ya kufanya uchunguzi na matibabu ya moyo.
Akizungumzia kuhusu ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema JKCI ni moja ya Taasisi inayoongoza katika nchi za Afrika Mashariki na kati katika kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo.
Dkt. Kisenge alisema Rais Mohamud alitembelea Taasisi hiyo kwaajili ya kuona namna ambavyo nchi ya Somalia itawapeleka wagonjwa wa moyo JKCI kupata tiba ya matibabu ya moyo.
“Nchi ya Somalia inawapeleka wagonjwa wengi wa moyo kwenda kutibiwa katika nchi za India, Ulaya na Marekani wakati huduma hii inapatikana nchini Tanzania, na ukiangalia nchi hizi ziko karibu hivyo basi itakuwa ni rahisi kwao kuwaleta wagonjwa kuja kutibiwa hapa kwetu”.
“Kuja kwa wagonjwa hawa kutaisaidia nchi yetu kukua kiuchumi kwani pesa zitakazopatikana zitawafikia watu wengi ikiwemo wamiliki wa hoteli ambako wagonjwa watalala pamoja na wafanyabiashara watakaowauzia vyakula na mahitaji mengine”, alisema Dkt. Kisenge.
Dkt. Kisenge alimshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuzidi kuimarisha mahusiano na nchi za nje ndiyo maana watu wengi wanakuja kuwekeza hapa nchi hata Taasisi hiyo imekuwa ikiwapokea wageni mbalimbali kutoka nchi za nje.
Akiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mhe. Rais Hassan Sheikh Mohamud pamoja na ujumbe wake aliambata na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu.
0 comments: