UJENZI WA BARABARA YA MSIKITINI SERIKALI YA AMANA, KATA YA ILALA

Mbunge wa Jimbo la Ilala na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe Mussa Azzan Zungu kwa kushirikiana na Mhe Saady Mohamed Khimji - Diwani Kata ya Ilala na Kamati ya Maendeleo Kata  amewaongoza wananchi wa Kata ya Ilala hususan Mtaa wa Amana kutembelea Barabara ya Msikitini kwa ajili ya kuanza taratibu za Ujenzi wa barabara hiyo kama inayoonekana pichani.


Mgeni Rasmi alikuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Alhaj Said Sultan Sidde.Pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama (CCM) na Serikali pia kulikuwa na Uongozi wa TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Kaimu Injinia Mkuu wa Mkoa Mr. Harrison.

Barabara hiyo yenye urefu wa  Mita 700 itajengwa kwa kiwango cha Lami, itawekwa Mifereji ya pembeni, kuwekwa Matuta na kuweka Taa za barabarani.
Mradi utagharimu kiasi cha shs Milion 760,000,000/=.

Mchakato wa kumpata mkandarasi umeshaanza leo rasmi na kuanzia Mwezi wa sita mwanzoni Kazi ya Ujenzi wa barabara hiyo na nyingine jimbo la Ilala zitaanza.

"Fedha za mradi zinatoka Serikali Kuu baada ya kuhidhinishwa na Rais wetu Mpendwa Mhe Samia Suluhu Hassan, tunamshukuru sana Mhe Rais Samia Suluhu kwa kuupiga Mwingi".

"Aidha nichukue fursa hii kutoka moyoni mwangu kumshukuru Mhe Zungu Mbunge kwa kupigania ili tupate fedha za Ujenzi wa barabara hiyo ya Msikitini Mhe Mbunge ni jembe linalima kusafisha njia hakika hakuna kama Mhe Zungu Ilala" ... Alisema Mhe Khimji.

UJENZI WA MIUNDOMBINU KATA YA ILALA UNAENDELEA...

KILA HATUA DUWA...
TOGETHER WE CAN DO MORE
Imetolewa na Ofisi ya Diwani Kata ya Ilala.

0 comments: