WAKULIMA WAKUMBUSHWA KUNUNUA MBOLEA KWA BEI ELEKEZI YA SERIKALI


Na Mwandishi wetu Mara.


IMEELEZWA kuwa wakulima wenye sifa za kununa mbolea ya ruzuku ya serikali wanatakiwa kununulia bei elekezi ya serikali ya shilingi alfu sabini tu.


Mkurugenzi wa kampuni ya serikali ya mbolea TFC,Lameck Borega aliwaambia waandishi wa habari kuwa serikali kwa kuona umhimu na kuwajali wakulima imeleta mbolea ya ruzuku ambayo itanunuliwa kwa bei elekezi ya shilingi alfu sabini tu kwa mfuko wa kilo hamsini na kama kuna mtu anauza zaidi ya hiyo bei taarifa zitolewe maeneo husika ili hatua zaidi zichukuliwe.


"Serikali ya Tanzania imeanziasha mkakati wa ugawaji ruzuku ya mbolea kwa lengo kuwakwamua wakulima na kuongeza kasi ya uzalishaji wa sekta hiyo inayotegemewa na wananchi wengi na Rais Samia Suluhu Hassani ameahidi kuikuza hiyo sekta"alisema Borega.


Moja kati ya malengo ya Wizara ya Kilimo kufikia mwaka 2030 yakiongozwa na Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuendelea kutoa ruzuku ya mbolea mpaka pale itakaposhuka bei kwenye soko la dunia ili kuwapunguzia gharama za uzalishaji wakulima nchini aliongeza kusema


Kwa upande wake Perusi Borega alisema kwa wasitani wa kutumia mbolea ya kupandia na kukuzia una uhakikka wa kuvuna tofauti na mtu ambaye hakitumia mbolea.


Perusi amewahimiza wakulima kuendelea kutumia mbolea kwasababu Ardhi imechoka na waanchane na kilimo cha kizamani cha mazoea kwa lengo la kupata mazao ya uhakika na kuongeza uzalishaji.


Mama huyo aliongeza kusema kuna haja wakulima kuzingatia ushauri wa wataalamu wa kilimo ambao wanatoa kwa ushauri kuufuata ili kunufaika na mbolea ya ruzuku.


Naye Meneja mkuu wa Chama cha ushirika cha wakulima wa Mara Cooperative union WAMACU,Samweli Gisiboye alisema mkakati wao nikuhakikisha kuwa wakulima wanapata mbolea kwa misimu yote miwili kwa hapa Tarime na mkoa mzaima wa Mara ili kiwango cha kilimo kupanda na wakulima kunufaika.


Meneja huyo alisema kwa mwaka huu kufikia Aprili 15,2023 wamegawa mbolea kwa wakulima mifuko 19800 sawa na tani 990 na kuwa wanamapungufu.


Meneja huyo aliongeza kuwa Chama chake kinafanya kazi na kampuni za mbolea kama vile OCPT ambayo imegawa mifuko 13200 sawa na tani 660 na hiyo ya TFCkampuni ya serikali ya Tanzania ambayo pia imegawa mifuko 19800 sawa na tani 990.


Gisiboye alimaliza kwa kusema wanamalengo ya kuondoa usumbufu kwa wakulima kutokana na kile alichokitaja kuwa wanamalengo ya kuuza mbolea kwa mkoa mzaima pamoja na viatilifu ikiwemo madawa ya kuulia wadudu waharibifu wa mazao ili chakula na mazao yaongezeka na wakulima kuinuka kiuchumi.

0 comments: