AJALI YA YAUA WAWILI MBOZI

   Watu wawili dunia papo hapo na kujeruhiwa Wilayani Mbozi, baada ya Lori la mizigo kufeli breki na kupoteza wakati likishuka katika mteremko wa Mlima Senjele ya pili barabara kuu ya Tanzania – Zambia (Tanzam) na kuyagonga malori mengine mawili.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Malya, amesema tukio hilo lilitokea Aprili 6.2023 baada ya aina ya Scania lenye namba T 413 BAE na Trela ​​lake T 444 BWF kufeli breki na kwenda kugonga malori mengine mawili na vifo.


Alisema lori hilo lilokuwa likiendeshwa na dereva Peter Simenda (39), Mkazi wa Jijini Dar es salaam ambaye kwa sasa amelazwa katika hospitali ya serikali ya Wilaya ya Mbozi, Mjini Vwawa baada ya kujeruhiwa vibaya, lililotokea Tunduma kuelekea Jijini Dar es saalam.


Kamanda Malya alisema baada ya dereva kushindwa kulimudu gari hilo alienda kuligonga Fuso lilokuwa mbele yake lenye namba za usajili T 418 AJR lilokuwa likitokea Wilaya ya Nkasi, Mkoani Rukwa kabla ya kuvamia Lori la mafuta lilokuwa likipanda kutokea Mbeya lenye namba T957 CFT na trela lake. namba T 513 BUS na vifo vya watu wawili.


Aliwataja waliofariki katika utingo wa Fuso, Liberatus Mfaume (40) mkazi wa Nkasi Mkoani Rukwa na Ally Yusufu ambaye ni dereva wa Lori la Mafuta.


Hata hivyo, Kamanda Malya alitoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Songwe kuacha kukimbilia kuiba mali badala yake wanatoa msaada kwenye matukio ya ajali.

0 comments: