Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
SIMBA
SC imethibitisha kumkosa Mshambuliaji wao raia wa Ghana, Augustine
Okrah baada ya kuumia katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Al Hilal SC
ya Sudan, mchezo uliopigwa kwenye dimba la Benjamin, jijini Dar es
Salaam na timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Klabu hiyo imeeleza kuwa Daktari wa
timu, Edwin Kagabo amesema kuwa Mshambuliaji Okrah atachukua muda kuanza
mazoezi na wenzake kuelekea kwenye mchezo wao dhidi ya Horoya AC kwenye
Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL), hatua ya makundi.
Hata
hivyo, Simba SC imethibitisha kuwa Wachezaji wake, Jean Baleke na Pape
Ousmane Sakho wanaendelea vizuri na wapo tayari kujiandaa na mchezo huo
dhidi ya Horoya AC. Baleke na Sakho walipata majeruhi kwenye mchezo huo
dhidi ya Al Hilal kwenye dimba la Benjamin Mkapa.
Mchezo
huo wa mzunguko wa Kundi C la Michuano hiyo utachezwa Februari 11, 2023
mjini Conakry nchini Guinea kwenye dimba la General Lansana Conté.
Baada
ya kumaliza mchezo wa kirafiki dhidi ya Al Hilal SC, Wachezaji wa Simba
SC walipewa mapumziko ya siku moja na watarudi kambini Februari 7, 2023
kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea mjini Conakry nchini Guinea kwa
ajili ya kipute hicho dhidi ya wenyeji Horoya AC kwenye Michuano hiyo ya
CAF CL.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: