DC MWANZIVA AITAKA ZIMAMOTO KUTOA ELIMU MASHULENI

Na. Mwandishi wetu, Njombe.

Mkuu wa wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva ameitaka idara ya zima moto wilayani humo kupita katika shule mbalimbali na kutoa elimu juu ya athari za majanga ya moto na namna ya kupambana nayo kitu ambacho kitasaidia wanafunzi kujikinga wenyewe na kuzuia uharibifu wa mali mbalimbali za serikali.

Mkuu huyo ameyasema hayo alipotembelea shule ya sekondari Lugarawa ambayo siku kadhaa zilizopita iliunguliwa bweni la wavulana na hivi karibuni tena kutokea kwa jaribio la kuunguza bweni la wasichana ambapo moto wake uliweza kuunguza vitanda vitatu, shuka na blanketi.

Kutokana na matukio hayo mkuu huyo wa wilaya ameunda kamati ya uchunguzi wa matukio hayo itakayo shirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kubaini vyanzo vya moto pamoja na wahusika wake kitu ambacho kitasaidia kuondoa hofu kwa wanafunzi na kukomesha matukio hayo.

" Kutokea kwa matukio haya kunaweza kujenga hofu kwa watoto wetu waliopo hapa shuleni, hivyo naomba vyombo vya usalama na kamati iliyoundwa mkafanye uchunguzi huu kwa haraka na kwa weledi ili tuweze kupata ufumbuzi wake". Amesema Mwanziva.

Sanjari na hilo pia mkuu huyo amewapongeza wale wote waliojitoa kwa michango ya ukarabati wa bweni hilo la wavulana lililoungua awali ikiwemo ofisi yake, Halmashauri na Mbunge wa jimbo la Ludewa kwani ukarabati huo umekwisha anza kwa kasi na wanatarajia wanafunzi kuanza kulitumia hivi karibuni.

" Nawasihi vijana wangu mtulie na muendelee na masomo yenu kama kawaida, haya maswala yatafanyiwa kazi ipasavyo hivyo ninyi someni kwa bidii ili mkuze kiwango cha elimu katika wilaya yetu". Amesema Mwanziva.

Deogratius Massawe ni mkuu wa polisi wa wilaya ya Ludewa amewaomba wananchi na wanafunzi kuonyesha ushiririkiano wao katika kubaini wahalifu huku Diwani wa kata ya Lugarawa Erasto Mhagama akiahidi kuwa bega kwa bega na vyombo vya usalama katika kutoa taarifa juu ya kitakacho hisiwa ama kubainika.



0 comments:

JK, CONDOLEEZZA RICE NA BILL GATES KUPAMBA SHEREHE ZA MIAKA 20 YA PEPFAR HUKO MAREKANI LEO

 

Rais wa Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa 66 wa Mambo ya Nje wa Marekani Dk. Condoleezza Rice na mfanyabiashara Bill Gates leo Februari 24, 2023 wataungana na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe. George W. Bush katika sherehe za kuadhimisha miaka 20 ya Mpango wa Dharura wa Rais wa Kupambana na UKIMWI (President’s Emergency Plan for AIDS Relief - PEPFAR) jijini Washington DC.


Sherehe hiyo, iliyoandaliwa na Taasisi ya George W. Bush itafanyika katika Taasisi ya Amani ya Marekani. Watatu hao watashiriki katika mjadala maalumu utaoendeshwa na Dkt. Rice kuhusu kuanzishwa kwa PEPFAR, mafanikio yake makubwa, na jinsi programu hiyo inavyofanikiwa katika nchi washirika na kwa sera ya kigeni za Marekani.

Mhe. Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, anatarajiwa kuhutubia kwa naiba ya Serikali katika kuadhimisha kumbukumbu ya PEPFAR.

Kwa Mujibu wa taarifa kutoka Taasisi ya George W. Bush, katika maadhimisho hayo, Mke wa Rais huyo Mstaafu wa Marekani George W. Bush, Bi. Laura Bush, atatoa maelezo mafupi na kuwatambulisha Tatu Msangi na Faith Mang'ehe, Mabalozi wa Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation kutoka Tanzania waliohudhuria wakati wa kutolewa hotuba ya Hali ya Muungano (State of the Union) katika Congress ya Marekani, ambapo mpango huo wa PFEPFAR ulitangazwa rasmi mwaka 2008.

Taarifa hiyo inaeleza kwamba Bill Gates, ambaye ni mwenyekiti mwenza wa Taasisi ya Bill na Melinda Gates, ataungana na Bw. David J. Kramer, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Bush, kujadili jinsi modeli ya mafanikio ya programu ya PEPFAR imeweza kuitambulishadunia ushiriki wa Marekani katika afya na maendeleo ya kimataifa kwa upana zaidi.

"PEPFAR bila shaka ni mpango wa msaada wenye mafanikio zaidi wa Marekani kuwahi kutokea, ambao umeokoa maisha zaidi ya milioni 25 hadi sasa," alisema David J. Kramer, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Bush.

"PEPFAR pia imeimarisha mifumo ya afya, imeimarisha demokrasia, imesaidia ukuaji wa uchumi, na maendeleo ya juu ya haki za binadamu. Congress na watu wa Marekani wanapaswa kuendelea kuunga mkono PEPFAR hadi UKIMWI usiwe tishio tena.”

Washiriki wengine katika sherehe hizo ni pamoja. Ken Hersh, Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Kituo cha Rais cha George W. Bush; Wendy Sherman, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani; Balozi Dk. John Nkengasong, Mratibu wa Ukimwi Ulimwenguni wa Marekani na Mwakilishi Maalum wa Diplomasia ya Afya Duniani; Mheshimiwa Seneta Lizzie Nkosi, Waziri wa Afya wa Eswatini; Winnie Byanyima, Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS; Peter Sands, Mkurugenzi Mtendaji wa The Global Fund; na Dk. Wafaa El Sadr, Mwanzilishi na Mkurugenzi wa ICAP katika Chuo Kikuu cha Columbia.

Ingawa tukio ni mwaliko pekee, litatiririshwa moja kwa moja kwenye bushcenter.org/pepfarat20.

0 comments:

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

0 comments:

BMH, BOMBO KUENDESHA KAMBI YA HUDUMA MBALIMBALI ZA KIBINGWA JIJINI TANGA


Na Mwandishi wetu, Tanga

HOSPITALI ya Benjamini Mkapa (BMH) ikishirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo wanatarajia kufanya kambi ya huduma mbalimbali za kibingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo kuanzia February 27 hadi Machi 3 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga –Bombo Dkt Naima Yusuf (Pichani) alisema kwamba maandalizi ya kuelekea kambi hizo yanaendelea vizuri huku akieleza huduma za kibingwa zitakazotolewa.

Dkt Naima alisema huduma zitakazotolewa ni Upasuaji Mishipa ya Fahamu ,Mifupa, Mfumo wa Haja ndogo (Mkojo),Magonjwa ya ndani,Tiba ya Figo,Tiba ya Moyo kwa watoto na watu wazima.

Alizitaja huduma nyengine zitakazotolewa ni Magonjwa ya watoto Magonjwa ya macho,Tiba ya Kinywa na Meno pamoja na Magonjwa ya Uzazi kwa akina Mama.

Hata hivyo Dkt Naima alisema kwamba katika kambi hiyo wateja wa bima ambao watapokelwa ni wa Jubilee Insurance,Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Assemble Insurance na Strategis Insurance.

0 comments:

MKUTANO WA KWANZA SHAMBULIO LA MOYO WAFUNGWA JIJINI DAR ES SALAAM

 

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shakalaghe akimpa cheti cha kutambua umuhimu wake katika kutoa huduma za matibabu ya moyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. William Mahalu wakati wa kufunga mkutano wa kwanza wa shambulio la moyo uliofanyika katika Hoteli ya Ledger Plaza jijini Dar es Salaam

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shakalaghe akimpa cheti cha kutambua umuhimu wake katika kutoa huduma za matibabu ya moyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakati wa kufunga mkutano wa kwanza wa shambulio la moyo uliofanyika katika Hoteli ya Ledger Plaza jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shakalaghe akimsikiliza Afisa Mauzo kutoka kampuni ya usambazaji wa dawa ya SUN PHARMA Innocent Maro lipotembelea kuona huduma zinazotolewa na kampuni hiyo wakati wa kufunga mkutano wa kwanza wa shambulio la moyo uliofanyika katika Hoteli ya Ledger Plaza jijini Dar es Salaam
  Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Khuzeima Khanbhai akipokea cheti cha kushiriki kuandaa mkutano wa kwanza wa shambulio la moyo ulioandaliwa na Taasisi hiyo na kumalizika jana jijini Dar es Salaam
  Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Engerasia Kifai akipokea cheti cha kushiriki kuandaa mkutano wa kwanza wa shambulio la moyo ulioandaliwa na Taasisi hiyo na kumalizika jana jijini Dar es Salaam
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kusambaza vifaa tiba ya Computech Limited Sandip Datta akipokea cheti cha kutambua mchango wake katika kushirikiana na JKCI kufanikisha mkutano wa kwanza wa shambulio ya moyo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Dkt. Seif Shakalaghe wakati wa kufunga mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Ledger Plaza jijini Dar es Salaam.






Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya MOI. Dkt. Reuben Mutagaywa akipokea cheti cha kushiriki wakati wa kufunga mkutano wa Shambulio la moyo uliofanyika katika Hoteli ya Ledger Plaza jijini Dar es Salaam.
 Mwandishi wa habari kutoka ITV Agnery Myala akipokea cheti cha kukitambua chombo cha habari cha ITV kwa kushirikiana na JKCI kufanya kipindi cha kutangaza kuhusu ugonjwa wa shambulio la moyo  wakati wa mkutano wa kwanza wa shambulio la moyo ulioandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kumalizika jana jijini Dar es Salaam. Vyombo vingine vya habari vilivyopewa cheti kwa kushirikiana na JKCI kutangaza kuhusu shambulio la moyo ni pamoja na TBC, Channel 10, Star TV, Clouds TV, Azam TV na ZBC

 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kwanza wa shambulio la moyo wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano kabla ya kufunga mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Ledger Plaza jijini Dar es Salaam. (PICHA NA KHAMISI MUSSA NA JKCI)

Na Mwandishi wetu

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imetakiwa kuendelea kufanya mikutano inayotoa mafunzo kwa wataalam wa afya itakayosaidia kuweka mbinu za kujikinga na magonjwa yasiyo ambukiza pamoja na kutafuta namna ya kutatua magonjwa hayo.


Rai hiyo imetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shakalaghe wakati wa kufunga mkutano wa kwanza wa Shambulio la moyo uliofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Larger Plaza uliopo jijini Dar es Salaam.


Dkt. Shakalaghe alisema mkutano huo umekuwa wa faida kwa wataalam wa afya kwani sasa wataenda kuongeza jitihada za kuokoa maisha lakini pia kuwapa nafasi wananchi kutambua dalili za ugonjwa huo hivyo kuchukua hatua za haraka pale wanaposikia dalili za shambulio la moyo.


“Wizara ya Afya itahakikisha mikutano hii inafanyika kila mwaka kuwakusanya wataalam wa afya maeneo tofauti ya dunia ili kwa pamoja waweze kubadilishana ujuzi na kutatua tatizo la shambulio la moyo ambalo kwa sasa linaonekana kuongezeka”,


Akizungumza katika Mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema Mkutano wa kwanza wa shambulio la moyo umewahusisha wataalam wa afya 300 kutoka nchi mbalimbali kujadili namna ya kuwahudumia wagonjwa wanaopata shambulio la moyo kwani sasa limekuwa tatizo kubwa katika jamii.


“Tatizo la shambulio la moyo linasababisha vifo vingi, wagonjwa wenye matatizo ya moyo duniani wanakaribia milioni 17 lakini wale wanaopata mstuko wa ghafla wa moyo ni karibu milioni sita duniani kote na kati yao asilimia 15 hupoteza maisha yao”, alisema Dkt. Kisenge


Dkt. Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema shambulio la moyo hata hapa nchini lipo kutokana na mfumo wa maisha ya kila siku ikiwemo uvutaji wa sigara, kutofanya mazoezi, kula mlo usio na afya, kuwa na uzito uliopitiliza hivyo kupelekea matatizo ya moyo likiwemo shambulio la moyo.


“Mkutano huu umewakutanisha wataalam wa afya ili kuona ni kwa namna gani wataweza kuzuia tatizo la shambulio la moyo kwa kuwaelimisha wananchi kufika mapema hospitali kwasababu mtu akipatwa na shambulio la moyo anapaswa kufika hospitali mapema kwa ajili ya kupatiwa matibabu”,


“Tumeona tufanye mkutano huu uliowakutanisha wataalamu wa afya kutoka nchi za Marekani, Agentina, Misri, India, Sudani, Kenya, Tanzania na nchi nyinginezo kubadilishana ujuzi na kutengeneza mfumo wa kutambua matatizo ya moyo na kuwaelimisha wataalamu wengine ambao hawakupata nafasi kushiriki katika mkutano huu”, alisema Dkt. Kisenge


Dkt. Kisenge alisema dalili za mstuko wa moyo ni pamoja na kupata maumivu makali ya kifua yanayoenda hadi kwenye mkono na taya, kutokwa jasho jingi, kukosa nguvu na kushindwa kupumua vizuri hivyo kuwataka wananchi wanapopatwa na dalili hizo wafike kwa wataalam wa afya ili waweze kuchunguzwa na kupatiwa huduma kwa wakati.


Naye mshiriki wa mkutano huo Daktari bingwa wa magonjwa ya dharura na ajili kutoka hospitali ya KCMC Fransis Sakita aliipongeza JKCI kwa kufikiria kuandaa mkutano huo ambao ungepaswa kufanyika siku za nyuma kwani uhitaji wa taalama iliyotolewa katika mkutano huo ni hitaji kubwa kwa wataalam wa afya.


Dkt. Fransis alisema kwa upande wa KCMC asilimia 22 ya wagonjwa wa moyo waliowahi kuwaona walikuwa na tatizo la shambulio la moyo hivyo kuona kuna uhitaji mkubwa wa jamii kuufahamu vizuri ugonjwa huo ili waweze kujikinga.



“Katika Hospitali yetu mwanzo kulikuwa na uhaba wa vifaa vya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo lakini sasa hivi tumepata vifaa vya kutosha pamoja na elimu ya mara kwa mara hivyo kutuwezesha kutambua wagonjwa na kuwapatia huduma kwa wakati” alisema Fransis 

0 comments:

TUJITOKEZE KUPIMA VIPIMO MAGONJWA YA MOYO KATIKA TAASISI YA JKCI

Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt.Godwin Mollel akizungumza na washiriki wa mkutano wa kwanza wa shambulio la moyo unaofanyika katika Hoteli ya Ledger Plaza, Bahari Beach jijini Dar es Salaam. (PICHA NA KHAMISI MUSSA)
Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt.Godwin Mollel akitoa tuzo kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Laurance Museru  ya kutambua mchango wake wa kuanzishwa kwa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mkutano wa kwanza wa shambulio la moyo uliofanyika katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach, jijini Dar es Salaam.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Dkt. Maneno Mlawa akipokea tuzo kwa niaba ya Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Mhe.Dkt.Godwin Mollel ya kutambua mchango wake wa kuanzishwa kwa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mkutano wa kwanza wa shambulio la moyo uliofanyika katika Hoteli ya Ledger Plaza, Beach jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya JKCI Prof. William Mahalu.

Naibu Waziri wa Afya Mhe.Dkt.Godwin Mollel akitoa tuzo kwa Daktari bingwa wa moyo kutoka Chennai India Ulhas Pandurangi kwa ajili ya kumshukuru kwa kufundisha mfumo wa umeme wa moyo katika mkutano wa kwanza wa shambulio la moyo uliofanyika katika Hoteli ya Ledger Plaza, Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Jumla ya washiriki 300 wanahudhuria mkutano huo wa siku mbili ulioandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) Dkt.Johnson Lwakatare alipokea tuzo za waasisi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  akiwemo yeye kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Mhe.Dkt.Godwin Mollel wakati wa mkutano wa kwanza wa shambulio la moyo uliofanyika katika Hoteli ya Ledger Plaza, Bahari Beach jijini Dar es Salaam.

   Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kwanza wa shambulio la moyo unaofanyika katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Mhe.Dkt.Godwin Mollel akifungua mkutano huo
Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel akitoa tuzo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Mohamed Janabi ya kutambua mchango wake wa kuleta mafanikio ya tiba ya moyo nchini wakati wa mkutano wa kwanza wa shambulio la moyo uliofanyika katika Hoteli ya Ledger Plaza, Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa siku mbili umeandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo washiriki 300 kutoka ndani na nje ya nchi wanahudhuria mkutano huo.
Naibu Waziri wa Afya Mhe.Dkt.Godwin Mollel akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano wa kwanza wa siku mbili wa shambulio la moyo unaofanyika katika Hoteli ya Ledger Plaza, Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter Kisenge na Kushoto kwa Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi.

Na Mwandidhi wetu

NAIBU Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kupima ili kufahamu hali zao za magonjwa ya moyo ili kutambua tatizo mapema na kuweza kulizuia kabla ya madhara makubwa kutokea.


Mhe.Dkt. Mollel amesema hayo leo Februari 17, 2023 Jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa Mkutano wa kwanza wa Shambulio la moyo uliohudhuriwa na Madaktari wa magonjwa ya moyo na Wataalamu wengine wa masuala ya Afya nchini.


"Wito wangu ni kwamba, suala la kupima moyo lisiwe mpaka usikie tatizo, iwe ni wakati wote, ndio maana tunawataka Wataalamu watembee katika vituo mbalimbali vya Afya ili kuhakikisha wanapima Watanzania wanaofika katika vituo ili wapate kujua hali zao juu ya ugonjwa wa moyo”, alisema Mhe. Dkt. Mollel.


Sambamba na hilo Mhe. Dkt. Mollel alitoa rai kwa wananchi kujenga tabia ya kufanya uchunguzi wa magonjwa hususan magonjwa ya moyo mara kwa mara ili kufanya utambuzi wa mapema utaosaidia katika kutibu tatizo hilo.

Aidha Mhe. Dkt. Mollel alisema Rais Samia amehidhinisha fedha nyingi sana katika uwekezaji kwenye Sekta ya afya ili kununua vifaa tiba vya kisasa vinavyosaidia katika ufunguaji wa kifua kwa kiasi kidogo sana na kutibu tatizo la moyo hali iliyosaidia kupunguza muda wa mgonjwa kukaa hospitali kwa ajili ya matibabu.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema dhumuni la mkutano huo wa wataalamu wa masuala ya moyo ni kubadilishana uzoefu ili kujiimarisha katika matibabu ya magonjwa ya moyo nchini.


Alisema Duniani kote zaidi ya watu milioni sita hupata tatizo la mshtuko wa ghafla wa moyo ambalo linachangia vifo vingi kwa wananchi hivyo kuwataka kuchukuwa hatua mapema pindi watakapohisi kuwa na tatizo hilo.


Mbali na hayo Dkt. Kisenge alitoa  wito kwa wananchi kuepuka kula vyakula vinavyoweza kuchangia magonjwa ya mashambulio la moyo ikiwemo vyakula vya mafuta mengi, na kuepuka uvutaji wa sigara na unywaji pombe kupita kiasi na kufanya mazoezi walau mara tatu kwa wiki kwa dakika 30.


Mkutano huo wa siku mbilli wenye kauli mbiu isemayo shambulio la moyo ni hatari kwa maisha yako, wahi Hospitali umehudhuriwa na washiriki 300 kutoka ndani na nje ya nchi.

0 comments:

MAGAZETI YA LEO 16/02/23

 







0 comments:

RAIA WA BURUNDI APATATUZO YA MUHANDISI MWEUSI BORA MWAKA WA 2023

   George Ndayizeye, raia wa Burundi anayefanya kazi kwenye kampuni ya kutengeneza ndege ya Boeing yenye makao yake mjini Seattle hapa Marekani, alipata tuzo ya muhandisi bora mweusi mwaka wa 2023, kutokana na mchango wake wa kiufundi kwenye kampuni hiyo.


Mapema wiki hii, mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Boeing Stanley Deal aliandika kwenye Facebook “Hongera George Ndayizeye kwa kupata tuzo ya Walt W. Braithwaite Legacy Award” kwa mchango wako mkubwa wa kiufundi.


Ndayizeye mwenye umri wa miaka 41, mzawa wa mkoa wa kusini mwa Burundi wa Makamba, ni muhandisi kwenye kampuni ya Boeing, anayehusika na kuchunguza namna ndege zinavyotengenezwa.


Akizungumza na Idhaa ya Kirundi na Kinyarwanda ya Sauti ya Amerika Jumatano, alisema ‘nilipokea kwa fura kubwa tuzo hiyo.’


“Nilipata tuzo hiyo kutokana na ubunifu mpya na mchango mkubwa wa kiufundi kwenye utengenezaji wa ndege”, alisema.


Ndayizeye amesema alichangia katika utengenezaji wa ndege aina ya Boeing 787 na Boeing 777-9 na ndege nyingine itakayombeba Rais wa Marekani.

0 comments:

BEI ZA MAZAO ZIMEONGEZEKA, MAPATO YA SERIKALI YAMEPAA- WRRB

  Mkurugenzi Mtendaji wa BODI ya usimamizi wa Stakabadhi za ghala (WRRB) Asangye Bangu akizungumza ,wakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za bodi hiyo mbele ya waandishi wa habari leo Februari 15,2023,jijini Dodoma.


Na Mwandishi wetu, Dodoma

Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) imetaja mafanikio lukuki tangu kuanzishwa kwa Mfumo wa Stakabadhi za Ghalani ikiwemo ongezeko la bei za mazao, mapato ya mkulima na mapato ya 
Serikali kwa wastani wa asilimia 200% kutokana na urasimishaji, ongezeko la uzalishaji wa mazao kwa wastani wa asilimia 12% kwa mwaka,kichecheo cha ubora wa mazao yanayofikishwa sokoni,


Mafanikio mengine ni upatikanaji wa takwimu sahihi za mazao yanayopita kwenye Mfumo wa Stakabadhi za Ghala, ongezeko la mapato ya uhakika kwa Serikali Kuu na Serikali Mitaa na kukuza huduma za fedha vijijini,kufanikisha uanzishaji wa Soko la Bidhaa Tanzania.

Mafanikio hayo yametajwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Asangye Bangu alipokuwa akielezea utekelezaji wa majukumu ya Bodi katika mkutano na vyombo vya habari Februari 15, 2023 kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO jijini Dodoma.

Aidha, Mkurugenzi huyo amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Mfumo 2007/08 hadi 2020/21 ukuaji wa uzalishaji umekuwa ukiongezeka kwa wastani wa 12% kwa mwaka ikilinganishwa na ukuaji wa 2% kwa mwaka kabla ya kuanzishwa kwa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala.

"Kwa mfano katika zao la Korosho mara baada ya kuanzishwa kwa Mfumo palikuwa na ongezeko la asilimia 164% la bei kutoka Ths 350.00 msimu wa 2006/07 hadi kufikia Tsh 925.00 msimu wa 2007/08 mwaka wa kuanza wa Mfumo; katika miaka minane tokea kuanzishwa kwa Mfumo 2007/08 hadi 2014/15 wastani wa ongezeko la bei kwa mwaka ulikuwa 25% kulinganisha na ongezeko la bei miaka minane kabla ya kuanzishwa kwa Mfumo la 12% kwa mwaka kaunzia mwaka 1998/99 hadi 2006/07," amebainisha Bangu

Mkurugenzi huyo amesema kuwa ili kuendana na kasi ya ukuaji wa teknojia Bodi imekuwa ikishirikiana kwa karibu na kuhamasisha bodi ya TEHAMA kukamilisha mifumo mipya na kuhamishia huduma za Bodi hiyo kwenda kidijitali.

Aidha, Bodi imeendalea juhudi za kuboresha Mfumo uliokuwepo wa kizamani wa Usimamizi wa ghala, ambapo kushirikiana na Bodi ya TEHAMA inakuja na Mfumo mpya wenye kuweza kurahisisha kazi za
maandalizi ya taarifa, utoaji stakabadhi na udhibiti wa matukio ghalani hivyo kupunguza muda wa michakato na kuongeza ufanisi na usalama wa mzigo.

"Majaribio ya Mfumo wa Maombi ya Leseni Mtandaoni
yamefanyika na mapendekezo ya maboresho yamepelekwa kwa programmers kwa ajili ya kufanyiwa kazi,"amesema Bangu

Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) ni taasisi chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara iliyoundwa kwa Sheria Namba 10 ya 2005 na Marekebisho Kifungu 4 Sura 339 R.E. 2016 iliyopewa majukumu chini ya Kifungu 5 (a-j) ikiwemo kutoa leseni kwa waendesha ghala, meneja dhamana na wagakuzi wa ghala;

 kuchapa and kuidhinisha vitabu vya Stakabadhi za Ghala, kusajili na kuingiza taarifa za wadau muhimu wa mfumo, kuwakilisha nchi katika masuala ya taifa na kimataifa yahusuyo Mfumo wa Stakabadhi za Ghala pamoja na majukumu mengine kama taasisi itakavyoelekezwa na Mhe. Waziri wa Viwanda na Biashara.

0 comments:

RAIS MWINYI AKUTUNA NA UJUMBE WA KAMPUNI YA PUMA AFRIKA.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (kulia) akimsikiliza Kiongozi wa Kampuni ya Puma Afrika Bw.Fadi Mitri  akiongoza Ujumbe wa Kampuni hiyo (hawapo pichani) ulipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa  mazungumzo yanayohusu  masuala mbali mbali ikiwemo uwekezaji wa Biashara ya Mafuta hapa Zanzibar leo 15/02/2023. (PICHA NA IKULU).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (kulia) akimsikiliza Kiongozi wa Kampuni ya Puma Afrika Bw.Fadi Mitri (wa pili kulia) akiongoza Ujumbe wa Kampuni hiyo ulipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa  mazungumzo yanayohusu masuala  mbali mbali ikiwemo uwekezaji wa Biashara ya Mafuta hapa Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akisisitiza jambo wakati alipokuwa na mazungumzo na Ujumbe wa Kampuni ya  Puma Afrika ukiongozwa na Kiongozi Mkuu Bw.Fadi Mitri (wa pili kulia) walipofika Ikulu Jijini Zanzibar,mazungumzo hayo yanahusu masuala mbali mbali ikiwemo   Bishara ya Mafuta hapa Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akizungumza na  Ujumbe wa Kampuni ya  Puma Afrika ukiongozwa na Kiongozi Mkuu Bw.Fadi Mitri (wa pili kulia) ulipofika Ikulu Jijini Zanzibar,mazungumzo hayo yaliyogusa masuala mbali mbali ikiwemo uwekezaji   katika Bishara ya Mafuta hapa Zanzibar.

0 comments: