NAIBU WAZIRI IKUPWA ALIPOITEMBELEA TAASISI YA MIFUPA MOI NOVEMBAR 1, 2017

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Dkt. Respicious Boniface (kushoto) akimkaribisha  Naibu waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu Mh. Stella Ikupa (Mb)
 Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu Mh. Stella Ikupa (katikati) katika picha ya pamoja na wafanyakazi kitengo cha karakana ya viungo bandia wa Taasisi ya Mifupa, kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Dkt. Respicious Boniface
  Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu Mh. Stella Ikupa (katika) akizungumza na wazazi waliyokuwa wamekuja Klinik katika Taasisi ya Mifupa (MOI)
 Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu Mh. Stella Ikupa akiwasalimia wazazi na watoto wao  waliyolazwa katika Taasisi hiyo
 Muuguzi wa WOD ya watoto Sada Mbilinyi (wa kwamza kulia) akimpatia maelezo Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu Mh. Stella Ikupa akiwa amempakata mtoto Jamila  Abrahaman (1) akiwa na mama yake Rehema Hamisi (39) wa pili kulia na kuanzia kushoto ni Dkt. Samuel Swai na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dokt. Respicious Boniface



Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu Mh. Stella Alex Ikupa alitembelea Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na kukagua karakana ya kutengenezea viungo bandia (Orthopaedic workshop) na wodi ya watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi.

Katika ziara hiyo Mh. Ikupa amepata taarifa ya utendaji wa kitengo cha viungo bandia na namna kinavyowajibika kuwasaidia walemavu hasa wale wa hali chini. Mh. Ikupa amesema ameamua kuitemebelea MOI kwakua ni Taasisi ambayo inashughulika na walemavu ili kukagua upatikanaji wa vifaa, gharama zake na kama walemavu wanaweza kumudu gharama hizo.

“Nimewatembelea ili kuangalia changamoto mlizonazo katika kuwahudumia walemavu ili tushirikiane kuzitafutia majawabu, Pia, nimekuja kuwasalimia kwani nimekua nikipata huduma (MOI) tangu nikiwa mtoto” alisema Mh. Ikupwa.

Awali Mkuu wa Karakana ya Viungo bandia ya MOI Bi Leah Mamseri, alimueleza Mh. Ikupa kwamba Taasisi inakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa vifaa vya kutengenezea viungo bandia kwani havipatikani hapa Tanzania na hivyo Taasisi inalazimika kuvinunua nchini ujerumani kwa gharama kubwa na hivyo kufanya viungo hivyo kupatikana kwa bei ya juu.

Pamoja na changamoto nyingi zilizotajwa Mh. Ikupa ameshauri Taasisi kutafuta namna ya kuvinunua vifaa hivyo kutoka nchi nyingine ambazo bei zake ziko chini ili watanzania wavipate viungo hoivyo kwa bei nafuu. Pia, ameahidi kuliwasilisha jambo hilo kwenye ngazi za juu ili Serikali iangalie uwezekano wa kuanzishwa kwa kiwanda cha kutengeneza vifaa hivyo hapa nchini ili walemavu wanufaike zaidi

0 comments: