WAASI WA KIKRISTO WAUA WAISLAMU 25 JAMHURI YA AFRIKA YA KATI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 4:44 PM
Magaidi wa Anti Balaka wakiwatishia kuwakata vichwa Waislamu Jamhuri ya Afrika ya Kati
Waasi wa Kikristo wenye mfungamano na genge
la kigaidi la anti-Balaka wameua Waislamu 25 ndani ya msikiti katika mji
wa Kembe wa kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Abdourahman Bronou, mkuu wa baraza
la wazee katika mji wa Kembe amethibitisha habari hiyo na kusema kuwa,
waasi hao waliuzingira na kuushambulia msikiti huo mapema Jumatano
asubuhi.
Akizungumza Ijumaa, Bornou ameongeza
kuwa, katika hujuma hiyo ya kigaidi Imamu wa msikiti na naibu wake
walikuwa miongoni mwa waliouawa. Wakuu wa mji huo wametangaza siku tatu
za maombolezo.
Machafuko huko Jamhuri ya Afrika ya Kati
(CAR) yalizuka mwaka 2013, baada ya waasi wa Seleka kumuondoa
madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo, François Bozizé. Baada ya rais
Mwislamu, Michel Djotodia kuchukua mamlaka, waasi na magaidi wa Kikristo
wenye misimamo ya kufurutu ada wa Anti-Balaka walianzisha mauaji ya
kimbari dhidi ya jamii ya Waislamu, ambapo maelfu ya Waislamu waliuawa
na wengine wengi kuwa wakimbizi.
Djotodia alilazimishwa na nchi za
eneohilo kujiuzulu mwezi Januari mwaka 2014 na hapo mauaji ya Waislamu
yakashika kasi zaidi. Kabla ya kuanza mgogoro huo, mji mkuu wa Jamhuri
ya Afrika ya Kati, Bangui, ulikuwa na Waislamu 130,000 lakini hivi sasa
taarifa zinasema idadi hiyo ni chini ya 1,000.
Aidha watu zaidi ya 400,000, wengi wao
wakiwa ni Waislamu wamelazimika kukimbia makazi yao huku wengine milioni
2.7, au nusu ya watu wote CAR wanahitaji msaada. Mauaji ya Waislamu CAR
yanajiri licha ya kuweko askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani
nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: