MWENYEKITI (CWT) MUFINDI OBI KIMBALE WALIMU TUNAISHI KWENYE MAPAGALE TUNAOMBA VIWANJA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 10:02 PM
Na Fredy Mgunda,Mufindi
Chama
cha walimu wa Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimemuomba
mkurugenzi kuwakopesha viwanja walimu ili kujikwamuamua na mazingira
magumu wanayokumbana katika nyumba wanazoishi.
Hayo
yalisemwa na mwenyekiti chama cha walimu wa Tanzania (CWT) wilaya ya
Mufindi Obi Kimbale alisema kuwa walimu wamekuwa wakiishi katika nyumba
chakavu au mbali na mazingira ya shule kitu kinachosababisha kushuka kwa
uwezo wa walimu kufundisha.
Kimbale
alisema kuwa walimu hawana pesa za kununua moja kwa moja viwanja hivyo
kwa njia ya kuwakopesha inawezekana kutokana kuwa ni waajiliwa wa
serikali na mishahara yao inajulikana na ni rahisi kuresha mkopo huo.
“Sisi
walimu ukitaka kujua mimi nalipwa shilingi ngapi ni rahisi tu kwa kuwa
mishahara ya serikali mara nyingi inajulikana hasa pale mtumishi
unapoenda kukopa mahali ndio maana tunaiomba serikali itusaidie kukopa
viwanja kuwa kuwa tunauwezo wa kulipa kwa awamu tatu” alisema Kimbale
Aidha Kimbale aliwatupia lawama maafisa elimu na walimu wakuu wa shule kwa kuwanyima ruhusa bila kuwa na sababu maalum.
“Wakurugenzi
amekuwa ametoa kibali upewe ruhusa lakini viongozi waliochini ya
mkurugenzi wanatuwekea vipingamizi ambavyo havieleweki kitu kinachozua
utata mkubwa baina ya viongozi na walimu ambao sio viongozi” alisema
Kimbale
Kimbale
alimpongeza wakurugenzi wa halmashauri ya mufindi na mji wa mafinga kwa
kuwajali walimu kwa kuwapa ruhusa pale inapotakiwa tofauti na hali
ilivyo kwa hawa viongozi wa chini yake.
“Unakuta
siku ya wanawake duniani au siku ya walimu duniani bado walimu
wananyimwa ruhusa wakati muda huo mkurugenzi amewaruhusu walimu
kuhudhuria sherehe hizo kitu kinachoongeza ukakasi baina ya watendaji wa
nafasi za juu na watendaji wa nafasi za chini” alisema Kimbale
Kimbale
aliwapongeza walimu wa manispaa ya Iringa kwa kuendelea kufanya kazi
kwa kujituma licha ya kukumbana na changamoto mbalimbali ikiwepo
kunyimwa ruhusa.
Akijibu
hoja hizo mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Williamu alisema haelewi
kwanini mara kwa mara swala hilo linakuwa linajirudia maana
tulishalitafutia ufumbuzi hapo awali.
Sasa
naenda kuandika barua rasmi kwa wakurugenzi ili kutatua kabisa tatizo
hilo maana hata kwangu imekuwa kero na mwazoni nilijua wakuu wa shule
ndio tatizo kumbe maafisa elimu ndio tatizo naenda kulishughulikia kwa
haraka sana swala hili” alisema Williamu
Williamu
aliwataka maafisa elimu na wakuu wa shule wote wa wilaya ya Iringa
kuwapa ruhusa walimu pale ambapo wanapata matatizo maana hakuna haja ya
kumnyima ruhusa mtu akiwa anashida na watakiwa kuzifahamu siku za
kitaifa ambazo ni lazima walimu wahudhurie wanapaswa kutoa ruhusa bila
kipingamizi.
“Kunasiku
kama siku ya mwalimu,siku ya wanawake na siku nyingine za kitaifa
walimu wanapaswa kupewa ruhusa kwenda kuhudhuria tukio hilo kutokana na
umuhimu wake” alisema Williamu
Williamu
alisema kuwa mkurugenzi ndio mwajili sasa hao maafisa elimu na wakuu wa
shule wanatoa wapi hiyo jeuri ya kuwanyima ruhusa ambayo viongozi wa
ngazi za juu wanajua kuwa kunakitu kinafanyika cha taifa.
Williamu
aliwataka viongozi wa walimu kuandika barua ya kuomba viwanja ili
waweze kulishughulikia swala hilo likiwa kwenye maandishi.
“Andikeni
barua yenye idadi na majina ya walimu wanaotaka viwanja ili kuondoa
kasumba ya kusema wanaotaka ni kikukindi cha walimu wachache tu na bila
kufanya hivyo swala lenu la kuomba viwanja litakuwa gumu kulitafutia
ufumbuzi” alisema Williamu
Williamu
aliwaomba walimu wawewavumilivu katika kipindi wacholishughulikia swala
hilo kwa kuwa sio jambo la kukurupuka linahitaji utulivu wa kutosha ili
kufanikishwa swala walimu kupata viwanja.
Naye
afisa elimu wa wilaya ya Mufindi alisema kuwa watawatafuta hao maafisa
ambao wanawanyima ruhusa walimu wakati swala hilo lilishatafutiwa
ufumbuzi.
“Jamani
sisi huku sheria tulishaiweka kwenye matukio muhimu ya kitaifa walimu
wapewe ruhusa sasa sijui ili sawala limetoka wapi naomba nikitoka hapa
nitazungumza na wakuu wa shule pamoja na maafisa elimu wenzangu”
mkuu
wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Williamuakizungumza na waandishi wa habari
wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya
Mufindi mkoani Iringa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: