Mstahiki Meya wa manispaa ya kinondoni Benjamin Sita
Azindua huduma ya kipesa ya “DCB JIRANI” na “DCB PESA” sambamba na
Makumu mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Pro. Lucian Msambichaka(kulia)
na mkurugenzi mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa Katika kuboresha huduma za
kibenki, Benki ya DCB sasa imeanzisha huduma za kibenki kwa njia ya
Mawakala (DCB Jirani ) ambapo itarahisisha upatikanaji wa huduma ya DCB
PESA, kupata huduma za kibenki kwa wepesi kwa njia ya simu za mkononi.
Ofisa wa DCB Pesa bwana Boniphace Asenga amesema Benki hiyo
sasa imewasogezea wateja wake waliopo mikoani huduma hii huku zaidi ya
mikoa 20 itanufaika na huduma hii, Mikoa ambayo itafikiwa na huduma hii
ni pamoja na Dar es Salaam, Pwani, Arusha, Mwanza, Iringa, Mbeya,
Njombe, Makambako, Tanga Mjini, Korogwe, Mombo, Morogoro Mjini, Kilosa,
Kilombero, Mikumi, Ifakara, Mtwara, Babati, Manyara, Dodoma Mjini,
Kibaigwa, Kondoa, Mpwapwa, Bahi, Chamwino na Kongwa.
Bwana Asenga amesema kuwa benki yao sasa inafikisha jumla ya
mawakala 700 ambao watatoa huduma hizo za kifedha katika kila mkoa Aidha
ameongeza kuwa Benki ya DBC pia inatoa nafai za kibiashara kwa
wafanyabiashara wanaotaka kuwa mawakala katika mikoa tajwa hapo
kujitokeza ili waweze kupatiwa uwakala kwa lengo na kufikisha huduma kwa
karibu zaidi kwa wateja wao kote nchini.
DCB Pesa inamrahisishia mteja kupata huduma za kibenki kupitia simu
yake ya mkononi popote alipo ikiwa ni pamoja na Kulipia bili kama vile
Luku, Maji, DSTV, Startimes, AzamTV, Zuku, TTCL na Smile, Kuhamisha pesa
kwenda kwenye mitandao ya simu kama M-Pesa, Tigo pesa, Airtel Money na
Halo Pesa, Kuongeza salio na kununua vifurushi vya muda wa maongezi,
Kutuma pesa kutoka akaunti moja kwenda akaunti nyingine pamoja na Kuweka
fedha kwenye mtandao wako wa Simu
0 comments: