Waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa amesema kuwa
anawakaribisha Chadema wale wote waliokatwa CCM. Katika taarifa yake kwa
vyombo vya habari leo Alhamisi, Lowassa amesema, “nimesoma na kusikia
baadhi ya waliokuwa viongozi katika Chama Cha Mapinduzi wamekatwa ama
kutetea nafasi zao au kugombea, kwa sababu mbalimbali. Na jina langu
limekuwa likiendelea kutajwa tajwa humo,
Mimi nawaambia hawa Watanzania wenzetu waliokatwa huko
CCM nawakaribisha huku Ukawa wafurahie demokrasia. Huku niliko kuna
maisha mazuri ya kisiasa, uhuru wa fikra na demokrasia halisi.” Lowassa
amesema Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere alisema ni wakati muafaka
kwa Tanzania kuwa na mfumo wa vyama vingi, pamoja na kwamba maoni ya
Watanzania wengi wakati ule kupitia tume ya Nyalali(Jaji Francis) kutaka
kuendelea na mfumo wa chama kimoja.
Nataka kuwakumbusha Watanzania wenzangu hawa, uamuzi ule wa Baba wa
Taifa, ulilenga kuwapa Watanzania demokrasia ya kuwa na uwanja mpana wa
kufanya siasa,” “Mimi nimetumia fikra hizo za mwalimu na hakika hivi
sasa ninafurahia demokrasia halisi huku niliko. Kwa wote waliokatwa na
wanahisi wameonewa waondokane na unyonge wa fikra kudhani kuwa bila CCM
hakuna maisha…
waje huku tufanye siasa kwa manufaa ya wananchi wetu.” Lowassa
amewaomba wanaChadema wenzake kuwapokea kwa mikono miwili na wale
wanaoendelea kubaki huko CCM waendelee kushikamana hadi uchaguzi mkuu
ujao 2020 ambapo upinzani utakapoonyesha makucha yao. “Vitisho na nguvu
ya dola inayotumika kujaribu kutunyamazisha sisi wa upinzani isiwatishe
wala kuwaongofya hata mara moja.
0 comments: