Mkurugenzi
wa Huduma za Tiba katika hospitali hiyo, Dk. Hedwiga Swai akisisitiza
watu kujitokeza kupima afya ili kuthibiti homa ya ini pamoja na magonjwa
mengine.
Baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo wakiwamo madaktari na wauguzi wakifuatilia kongamano hilo.
Daktari
Bingwa wa Magomjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini, John Rwegasha wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza katika kongamano jinsi
ya kudhibiti na kutibu magonjwa ya mfumo wa chakula na ini.
Baadhi ya madaktari, wauguzi wa hospitali hiyo na watumishi wengine wakiwa kwenye kongamano hilo leo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini, Priumus Saidia akizungumza kwenye kongamano hilo leo.
Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) imetoa ripoti ya robo mwaka tangu ianze
kufanya uchunguzi wa Virusi vya Homa ya Ini ( Hepatitis B) na kutoa tiba
ya ugonjwa huo kwa kutumia dawa ya Tenofovir .
Akitoa
taathimini hiyo leo jijini Dar es salaam, Daktari Bingwa wa Magonjwa
ya Ini na Matumbo John Rwegasha amesema muamko ni mkubwa ambapo katika
kipindi cha robo mwaka , Hospitali ya Taifa Muhimbili imesajili
wagonjwa 950 .
Akifanunua amesema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu idadi ya wagonjwa itaongezeka na kufika 1800 .Hata
hivyo kati ya hao , wagonjwa 540 ndio wamerudi tena Hospitalini kwa
ajili ya kuendelea na mchakato wa uchunguzi huku wagonjwa wengine
wakishindwa kufika kutokana na sababu za mbalimbali hususani za kiuchumi
, nakuongeza kwamba waliopo kwenye tiba ni wagonjwa 40.
‘’Idadi
ya wagonjwa imeongezeka mara dufu hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu
watafika wagonjwa 1800 lakini pamoja na changamoto hiyo hatuwezi
kusimamisha huduma tutaendelea kutoa huduma kwani kwa upande wa dawa
tumejidhatiti kwa miaka mitano , wagonjwa hawa wanatakiwa wafanyiwe
uchunguzi ili aanze kutumia dawa lakini si wote wanaohitaji dawa’’
amesema DK. Rwegasha.
Kwa
upande wake Dk. Tuzo Lyuu amesema tatizo la ugonjwa huo ni kubwa kwani
tafiti ambazo zimefanyika , watu wanaoenda kuchangia damu asilimia nane
wanatatizo hilo na kusisitiza kuwa tatizo hilo si la Tanzania pekee
bali hata kwa nchi zingine zinazoendelea.Kwa mujibu wa Dk. Lyuu kwa
sasa tatizo la Homa ya Ini (Hepatitis B) ni kubwa kuliko Ukimwi .‘’ Hapa
MNH watu tunaowaona ni vijana na watu wazima na wanaume ndio wengi
ingawa hakuna takwimu halisi’’ amesema Dk. Lyuu.
Ugonjwa
wa Homa ya Ini unasababishwa na Virusi viitwavyo Hepatitis B na
maambukizi ya ugonjwa huo yanashabiana na njia ya maambukizi ya Vrusi
vya Ukimwi kama vile kufanya ngono zisizo salama, kuchangia sindano au
vikatio, kupewa damu isiyopimwa , kupitia uzazi wa mama na mtoto hasa
wakati wa kujifungua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: