Rais mstaafu wa awamu ya nne
dk.Jakaya Kikwete ,akitoka kutembelea bweni alikuwa analala wakati
akisoma shule ya sekondari Kibaha mwaka 1966-1969, wakati wa mahafali ya
50 ya kidato cha nne shuleni hapo,huku akiwa ameambatana na viongozi
mbalimbali akiwemo mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wa pili
kushoto,na viongozi wa shule ya sekondari Kibaha na shirika la elimu
Kibaha.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Baadhi ya wahitimu wakiimba wimbo maalum katika mahafali hayo.
Rais mstaafu wa awamu ya nne
,Dk.Jakaya Kikwete, akipokea zawadi ya picha aliyochorwa na mmoja wa
wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Kibaha, Mkoani Pwani,
wakati wa mahafali ya 50 ya wanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo
.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Rais mstaafu wa awamu ya nne
,Dk.Jakaya Kikwete, akizungumza wakati wa mahafali ya 50 ya wanafunzi wa
kidato cha nne ya shule ya sekondari Kibaha mkoani Pwani ,shule ambayo
aliwahi kusoma mwaka 1966-1969 .(picha na Mwamvua Mwinyi)
Rais mstaafu wa awamu
ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne shule ya sekondari Kibaha, wakati
wa mahafali ya 50 ya kidato cha nne shuleni hapo .(picha na Mwamvua
Mwinyi)
Pic 4
Rais mstaafu wa awamu
ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa
shule ya sekondari Kibaha, wakati wa mahafali ya 50 ya kidato cha nne
shuleni hapo .(picha na Mwamvua Mwinyi)
………………………………………………………………..
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Rais mstaafu wa awamu
ya nne ,dk.Jakaya Kikwete ,ametoa rai kwa wadau na viongozi ambao
wametokea katika chimbuko la shule ya sekondari ya Kibaha;” ,Kuangalia
namna ya kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa ambayo inasababisha
mlundikano wa wanafunzi madarasani.
Aidha amesema mbegu ya
kuwa yeye mwanasiasa ilipandwa shuleni hapo, baada ya kuchaguliwa
kiongozi wa baraza la shule kutokana na harakati zake za kutetea haki za
wanafunzi .
Dk.Kikwete aliyasema
hayo shirika la elimu Kibaha ,wakati wa mahafali ya 50 ya wanafunzi wa
kidato cha nne shule ya sekondari Kibaha ambako alipata elimu yake ya
sekondari mwaka 1966 hadi 1969.
Alisema ,atashirikiana na wadau mbalimbali kuona namna bora ya kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa madarasa .
Dk.Kikwete alisema ,
haipendezi na hajafurahishwa na hali ya miundombinu ilivyokuwa chakavu
hali inayoathiri mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji .
Rais huyo mstaafu wa
awamu ya nne ,alieleza changamoto hizo si sababu ya kushindwa bali
uwepo wa changamoto huongeza umakini ,bidii na ubunifu ili kukabiliana
nazo .
Alifurahishwa kusikia
serikali imejizatiti kukarabati shule kongwe nchini na shule ya
sekondari Kibaha ikiwemo ,;”Hivyo aliwaomba wavute subira maana
kulingana na kasi ya awamu ya tano anaamini ukarabati huo hautachelea .
Alielezea ,shirika la
elimu Kibaha ni chemchem ya elimu bora ,iliyozaa viongozi bora na
wataalamu wanaoliletea sifa nzuri taifa .
Dk.Kikwete alieleza
kuwa ,pia shirika hilo ni tunu muhimu iliyoachwa na muasisi na baba wa
taifa mwalimu Julius Nyerere kwa kushirikiana na nchi za Nordic .
“Jamii ya watanzania
inaendelea kushuhudia matokeo mazuri ya shule ya sekondari Kibaha katika
mitihani ya kitaifa kwa kidato cha nne na cha sita “
“Pia ushindi na tuzo
katika nyanja zingine na mafanikio kwa wanajumuia ya shule hii ni
ushahidi tosha kwamba ,shirika hili ni chemchemya elimu bora na
iliyozalisha wanasiasa,madaktari,maprofesa ,wataalamu na viongozi wa
juu” alifafanua dk.Kikwete .
Kuhusu miradi ya
uzalishaji kwenye shirika hilo ,alisema ni wazo la kulifanyia kazi
,itawasaidia kuwajengea vijana moyo wa kupenda kazi za mikono na
utakuwa mtaji .
Dk.Kikwete, aliwatakia
wahitimu mafanikio mema katika mtihani wa kidato cha nne kitaifa
unaotarajiwa kuanza kufanyika octoba 30 mwaka huu .
Kabla ya shughuli ya
mahafali hayo, alipata fursa ya kwenda kutembelea bweni alilokuwa
akilala ,maktaba ,maabara na maeneo mengine shuleni humo .
Awali mwenyekiti wa
bodi ya shirika la elimu Kibaha, prof.Patrick Makungu ,alisema shirika
linakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundombinu na vifaa vya
kufundishia fani za ufundi .
Alieleza ,shirika hilo
ni taasisi ya kihuduma iliyoanzishwa miaka 54 iliyopita ,na jukumu lake
kubwa ni kupigana na kushindwa maadui ujinga ,maradhi na umasikini .
Prof .Makungu alisema
mkakati wao ni kuhakikisha wanatoa wanafunzi na wanavyuo wenye maarifa
,ujuzi na nidhamu katika elimu ya msingi ,sekondari ,ufundi stadi
,mafunzo maafisa tabibu na uuguzi .
Nae mwalimu Mkuu shule
ya sekondari Kibaha,Chrisdom Ambilikile alisema shule hiyo ipo vizuri
kitaaluma ambapo imekuwa ikifanya vizuri miaka 13 mfululizo sasa .
Alisema mwaka jana walipanda ufalu kitaifa kufikia nafasi ya 16 kutoka ya 69 hivyo wanatarajia kupanda zaidi .
Ambilikile alisema,
wanatatizo la upungufu wa madarasa matano ,ambao unasababisha
mlundikano wa wanafunzi katika vyumba vichache vilivyopo .
Shule hiyo, ilianzishwa
mwaka 1965 kwa msaada wa kifedha wa nchi za Nordic ikiwa na wanafunzi
110 kwa sasa ina wanafunzi 728 wote wakiume ,walimu 57 ,Na wanafunzi
wanaohitimu kidato cha nne mwaka huu ni 116 .
0 comments: