Mwezi wa Muharram ni mwezi wa rehema na
huruma na ambao unaweza kuyafanya makundi na madhehebu tofauti ya
Kiislamu kuwa na uhusiano mzuri wa kimaanawi.
Pamoja na hayo kuna makundi maovu
ambayo yameazimia kuleta mgawanyiko na hitilafu miongoni mwa jamii ya
Waislamu kwa kuendesha mauaji ya kutisha dhidi yao. Mlipuko wa kigaidi
uliotekelezwa katika mwezi wa Muharram nchini Saudi Arabia mwaka 2015 ni
mfano wa wazi kuhusiana na suala hilo. Mwaka 2015 kudi la kigaidi la
Daesh lilitoa taarifa likitangaza kuhusiana na tukio hilo la kigaidi
dhidi ya Mashia wa Saudi Arabia. Kundi hilo limehusika na matukio mengi
kama hayo nchini humo. Mwezi Mei mwaka 2014 magaidi wa kundi hilo la
kitakfiri walivamia msikiti mmoja wa Mashia katika mji wa Dammam na
kuwaua kinyama watu wanne waliokuwa wakitekeleza ibada zao kwenye
msikiti huo. Katika tukio jingine kama hilo katika mji wa Qadeeh ulio
karibu na mji wa Qatif magaidi hao walifanya shambulio jingine la
kinyama na kuwaua Mashia 24 wasio na hatia. Kabla ya hapo Shirika la
Msamaha Duniani, Amnesty International, lilikuwa limeutaka utawala wa
Saudia kuchukua hatua za lazima kwa ajili ya kuwalinda Mashia
waliowachache nchini humo kutokana na mashambulio ya mara kwa mara ya
magaidi wa Daesh, likisema kuwa mashambulio kama hayo dhidi ya misikiti
ya Mashia yalikuwa yameongezeka kwa kiwango cha kutisha.
Mashia wa Saudia wakifanya maandamano dhidi ya mauaji na ukandamiza wa utawala wa nchi hiyo
Jambo la kushangaza ni kuwa mashambulio
kama hayo ya kigaidi yamekuwa yakiripotiwa katika maeneo ambayo Waislamu
wa madhebu tofauti ya Kiislamu wamekuwa wakiishi pamoja kwa amani,
maelewano na ushirikiano. Matukio kama hayo pia yamekuwa yakiripotiwa
kwa wingi katika maeneo tofauti ya Pakistan na hasa katika mwezi kama
huu mtukufu wa Muharram. Kuhusiana na suala hilo, Majid Hairani,
mwandishi wa shirika la habari la Sky News anasema: ''Daima
Pakistan imekuwa ikikabiliwa na changamoto katika mwezi wa kwanza wa
Hijiria. Mwaka 2013 ndugu wawili wa Kisuni Sami' ad-Deen na Swalah
ad-Deen wakazi wa Pishawar ambao waliamua kushiriki katika maombolezo ya
Muharram mjini humo waliuawa. Magaidi ambao hawakuvumilia kuona ishara
hiyo ya udugu na umoja kati ya Waislamu, waliamua kuwaua ndugu wawili
hao kwa kuwafyatulia risasi. Vilevile mwaka 2012 Mawahabi waliua
waombolezaji 28 na kuwajeruhi wengine 70 katika maombolezo ya Muharram
kupitia shambulio la kujilipua kwa bomu. mwaka 2013 kundi jingine la
kigaidi la Taliban la nchini Pakistan lilitangaza kuhusika na milipuko
hiyo ya kufuatana iliyotokea katika Husseinia na mikusanyiko ya
waombolezaji wa Kishia katika miji ya Karachi na Rawalpindi. Allama
Rajah Nassir Katibu Mkuu wa chama cha Majlisi ya Umoja wa Waislamu wa
Pakistan na pia Altaf Hussein, Mkuu wa Harakati ya Kitaifa ya Umoja ya
Pakistan walilaani vikali mashambulio hayo na kuitaka serikali
iwadhaminie waombolezaji usalama.'' Mwisho wa kunukuu.
Moja ya milipuko ya kigaidi Pakistan
Mwezi wa Muharram kwa Waislamu ni mwezi
wa mapambano pia. Ni kutokana na ukweli huo ndipo tawala vibaraka
zikahofia mkusanyiko mdogo tu wa waomboleza wa mjuu wa Mtume Mtukufu
(saw). Huu ndio ndio ukweli mchungu unaowakabili pia wananchi wa
Bharain. Is'haq Anjazi, mtaalamu wa masuala ya kisiasa anasema: 'Kwa
mara nyingine tena watu wa Bahrain wameonyesha hasira zao kuhusiana na
uvunnjiwaji heshima maombolezo ya siku za Muharram unaofanywa na utawala
wa nchi hiyo, kwa kufanya maandamano dhidi ya utawala wa Aal Khalifa.
Askari usalama wa utawala huo wamekusanya mabango na maberamu yote
yanayohusiana na maombolezo ya Muharram. Utawala wa Aal Khalifa tokea
mwaka 2011 hadi sasa umekuwa ukikandamiza vikali malalamiko na
maandamano ya wapinzani na kubana kabisa shughuli zao za kijamii.
Utawala huo pia kufikia sasa umeua makumi ya wapinzani na kufunga jela
mamia ya wegine.'' Mwisho wa kunukuu.
Ama ni kwa nini wapinzani wa maombolezo
hayo ya kidini huingiwa na hofu na uoga kila yanapofanyika? Ni wazi kuwa
nguvu na nishati inayotokana na Muharram kwa ajili ya kuwaunganisha
Waislamu daima huwatia hofu wapinzani na hivyo kutaka mwenendo wake
ubadilishwe.
Maandamano ya Mashia wa Bahrain dhidi ya ukandamizaji wa serikali
Kuhusu hilo Adnan Sawajiri, mwanaharakati wa kisiasa anasema: ''Suala
la kuwepo madhahebu tofauti ni jambo linalokubalika katika Uislamu.
Pamoja na hayo, kuna makundi ambayo daima yanataka kuzua hitilafu
miongoni mwa Waislamu ili yapate kuendeleza siasa zao. Kitambo ni
wakoloni wa Uingereza na Ufaransa ndio waliokuwa wakiwasha moto wa
hitilafu hizo lakini hivi sasa ni makundi ya kitakfiri ndiyo yanayoua
Waislamu wa Shia na Suni kwa jina la 'Mwenyezi Mungu'." Kuna itikadi
mpya ambayo imejitokeza katika kipindi cha karne moja iliyopita ambayo
inakufurisha wengine kirahisi kabisa na kuua Waislamu wenzao. Bila shaka
mshindi wa mchezo huo hatari ni nchi za kibeberu na maadui wa Uislamu." Mwisho wa nukuu.
Pamoja na hayo, sasa watu wote
wanafahamu kwamba Muharram ni harakati ya kisiasa na kidini iliyo na
lengo maalumu la kudhihirisha uwezo na nguvu ya Kiislamu, ambayo licha
ya kukabiliwa na vitendo vya ugaidi wa kujilipua kwa mabomu, lakini
vitendo hivyo vimeshindwa kabisa kupunguza matokeo yake chanya ya kuleta
umoja na mshikamano kati ya Mashia na Masuni.
0 comments: