MKURUGENZI MTENDAJI AFUNGA SEMINA YA UJASILIAMALI KWA WANACHAMA WA TUGHE MOI

  Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface (kushoto) akizungumza na wanachama wa Tughe Tawi la Taasisi hiyo wakati alipokuwa akifunga semina ya ujasiliamali iliyoandaliwa na Chama Cha Wafanyakazi Tawi la Taasisi hiyo, Dkt.  Boniface aliwashukuru waandaaji na watoa mada wote kwa kuwapatia elimu hiyo na kuwaomba washiriki kuyashika yale waliyofundishwa na kuyaendeleza .(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
 Katibu wa Tughe Mkoa wa Iringa, Shadrack Mkodo (kulia) akizungumza Wakatialipokuwa akitowa mada ya ujasiliamali kabla ya kufungwa na Mkurugenzi wa taasisi ya (MOI) iliyofanyika Dar es Salaam jana
 Washiriki wakisikiliza kwa umakini
   Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface (wa tatu kulia) akiandika jambo wakati Katibu wa Tughe Mkoa wa Iringa, Shadrack Mkodo (pichani hayupo) alipokuwa akitowa mada katika Ukumbi wa Taasisi hiyo.
 Washiriki
 Mwenyekiti wa Tawi la Tughe (MOI), Privatus Masula (kushoto) akizungumza jambo kabla ya kufungwa semina hiyo na    Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Boniface (wa tatu kushoto waliyokaa)
 Mwenyekiti wa Tawi la Tughe (MOI), Privatus Masula, akizungumza na wandishi wa habari alisema, anapenda kumshukuru Mungu na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo kwa kukubali kuwa Mgeni rami na kuwashukuru viongozo wote waliyowezesha kufanikisha kufanyika kwa semina hiyo ya ujasilia mali kwa wanachama wa Tawi la Tughe (MOI), Masula alisema.

Lengo lake nikuona wafanyakazi wanafanya kazi kwa kujituma kwa moyo mmoja ili kupelekea Taasisi kupata mapato na kuwezesha kupata maslahi kwa wakati nakuwahi mahala pa kazi na pia aliwaomba kwa wafanyakazi wote kujituma ili kuzalisha kiasi cha kutosha ili hata ikitokea kumwambia mwajiri aweze kuwa na kitu cha kutulipa.

Masula anawaomba washiriki hao kuweza kujitegemea katika kujiajiri kwa kufuga kuku ambapo mtu huyo anaweza kuchukuwa dakika 45 ambazo zinamtosha kuiendeleza miradi yake tofauti ya kwenda katika hospitali nyingine na kwenda kuumia kwa masaa mengine, pia Masula alisema.

Kuzingati mafunzo hayo waliyoyapata na kuwa ufugaji wa nyuki na kilimo cha kisasa kutoka kwa mtoa mada kuzingatia sana ili mfanyakazi aweze kujikwamua na isiwe kutegemea mshahara .

Masula alisema,  kulingana na mafunzo hayo mtu anaweza kujiajiri na kuajiri watu wengine kwakujipatia kipato nje ya mshahara na kutowa wito kwa Serikali katika sehemu zao za kazi, Serikali iweze kuwashawishi wafanyakazi sehemu zao za kazi wajiunge na vyama vyao vya wafanyakazi na vilevile Serikali ijaribu kuviwezesha vyama vya wafanyakazi pale wanapodai madai yao waweze kutimiziwa, aliendelea kwa kusema.

Mfano wapo wafanyakazi ambao hawajapata mafao yao na mtuhuyo kisha staafu kwa mujibu wa sheria na anaendelea kuambiwa asubiri kwa muda mrefu, hivyo naiomba serikali kulifanyia kazi kwa wafanyakazi wanao dai walipwe kwa wakati pia.

Naishukuru Taasisi ya MOI kwa mtu anaye staafu hupewa mkono wa kwaheri ambapo unamuwezesha kumsaidia huko anakokwenda.

Masula ajijibu swali aliloulizwa na mwandishi, hapa MOI kunadhana ya wananchi wanasema, wafanyakazi wanafanya kazi wanavyo taka je, unalizungumziaje? Masula alisema.

Naweza kusema hiyo ni dhana potofu na ninayoweza kusema ni potofu kaulihiyo na niyakupuuzwa na ni kwamba sikweli na kwa muda nilioingia madarakani sijasikia swala hilo kwa wafanyakazi wa Taasisi hii swala hilo halipo na tunajitahidi kupita katika kila Idara na pia MOI tunafanya kwa masaa kumi na mbili na wanafanyakazi kwa kujituma sana na hata ukipita na utawakuta kila mmoja mgonjwa yupo katika sehemu yake anayo tibiwa kulingana ugonjwa.



 Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface akizungumza na wandishi mara baada ya kufunga semina ya
ujasilia mali kwa wanachama wa Tawi la Tughe (MOI).

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dkt. Respicius (wa tatu kushoto) waliyokaa katika picha ya pamoja na  washiriki 





Katibu Tughe Mkoa, Gaudensi Kadyango (kulia) akizungumza na wanachama wa Tughe Tawi la Taasisi ya  (MOI) na kumshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo,chachu ya semina hii ni mwendelezo wa semina iliyofanywa Morogoro ilichukua makatibu wa mabaraza ya wafanyakazi, ikachukua wenyeviti wa chama cha wafanyakazi na ikachukua afisa utumishi  mmoja kila tawi kwa aliyeweza kushiriki
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dkt. Respicius (wa tatu kushoto) waliyokaa katika picha ya pamoja na  washiriki 

0 comments: