KONGAMANO KUBWA LA AFYA KWA WOTE KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 9:18 PM
WADAU wa
sekta ya afya, watafiti, wanazuoni na wataalamu wa masuala ya bima,
wanakutana jijini Dar es salaam kesho tarehe 4 Mei, 2017 kujadili suala
la Afya bora kwa wote katika kongamano litakalofanyika katika hoteli ya
bahari beach jijini dar es salaam.Kongamano
hilo kubwa kufanyika nchini linafanyika chini ya mwavuli wa ushirikiano
kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (Public Private Partnership)
linafanyika katika kipindi ambacho taifa linajiandaa kuhakikisha kila
mtanzania anakuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu kupitia bima
ya afya.
Mmoja wa
waandaji wa kongamano hilo Dk. Heri Marwa kutoka Shirika la PharmAcess
amesema kuwa jumla ya washiriki 250 kutoka makundi mbalimbali ya
kijamii, utendaji na usimamizi na wawakilishi kutoka Serikalini
wanatazamiwa kushiriki. Kongamano hilo limeandaliwa kwa pamoja kati ya
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA) na Shirika la PharmAccess
linalosimamia huduma ya Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa katika mikoa
ya Kilimanjaro na Manyara kazi ambayo PharmAcess wanafanya kwa
kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika mikoa hiyo.
Kwa
mujibu wa Dk. Heri lengo la kongamano hilo ni kujenga uelewa wa pamoja
kuhusu hatua iliyofikiwa na Serikali kuelekea afya bora kwa wote na
umuhimu wa wadau mbalimbali kuunga mkono jitihada hizo. Amesema pia
washiriki watapata fursa kubadilisha uzoefu katika maeneo muhimu ambayo
ndio dira kuu ya kuelekea afya bora kwa wote yanayohusu; kuongeza uwigo
kwa makundi mbalimbali hasa sekta isiyo rasmi, umuhimu wa huduma bora na
masuala ya TEHAMA pamoja umuhimu wa masuala ya utafiti.
Nchi
mbalimbali hasa barani Afrika zimekuwa zikikwama kutekeleza azma hii
kutokana na kukosekana kwa utashi wa kisiasa. Bahati njema hapa nchini
suala hili lina utashi mkubwa wa kisiasa. Kazi kubwa katika kongamano
hili itakuwa ni kubaini matarajio na changamoto na kueneza mifano bora
(best practises) inayotekelezeka wakati tukielekea kutekeleza azma hiyo
ya afya kwa wote alimalizia Dk Heri na kuwakumbusha washiriki wote
waliothibitisha kushiriki kuwahi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: