TUNAPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA KIMYA KIMYA: WAZIRI MKUU MAJALIWA

 
 NA K-VIS  BLOG
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amewaonya wanaojihusisha na uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya popote walipo, kuacha biashara hiyo kwani Tume ya Kudhibiti na Kuzuia Dawa za Kulevya ambayo yeye ni Mwenyekiti wake, inaendelea na kazi kimya kimya na kwa nguvu kubwa.
“Msidhani tumeacha kushughulika, hatutaki sifa, sisi tunafanya mambo kimya kimya, na usijaribu kukubali kubeba madawa, tutakutambua tu, tunaendelea kuwakabili vilivyo watu hawa.” Alisema Waziri Mkuu wakati akifungua kongamano la kidini linalojadili mmomonyoko wa maadili katika jamii, lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), kwenye ukumbi wa Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam jana, Aprili 24, 2017.
 Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Alhaji  Abubakary Zuberi akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majaliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam jana Aprili 24, 2017. 
 Kamishina Jenerali wa  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya, Nchini, Rogers Siyanga akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam. 
 Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majaliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam. 
 Waziri Mkuu, akisalimiana na Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Alhaji  Abubakary Zuberi 
 Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akisalimiana na Kamaishna Jenerali wa Tume ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)  kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam jana Aprili 24, 2017. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI  MKUU)

0 comments: