TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YATOA HUDUMA YA UPIMAJI WA MOYO KWA MTOTO ALIYEPO TUMBONI KWA MAMA YAKE (FETAL ECHO)
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 1:48 PM
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa
watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Naiz Majani akimpima Mama
Mjamzito moyo wa mtoto aliyepo tumboni ili kuangalia kama una magonjwa au
la. Mwishoni kwa mwaka jana Taasisi hiyo iliwapima wajawazito 25 kati ya
hao watano watoto wao walikutwa na matatizo ya Moyo.(PICHA NA ANNA NKINDA – JKCI)
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi akiongea na waandishi wa habari kuhusu kazi
mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ikiwemo upimaji wa kina mama wajawazito
moyo wa mtoto aliyepo tumboni (Fetal ECHO) ili kuangalia kama una
magonjwa au la. Kutolewa kwa huduma hiyo kutasaidia kufahamu afya ya mtoto
aliyepo tumboni ikiwa ni pamoja na hali ya moyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: