PROFESA MKUMBO ATINGA DAWASCO AWAMWAGIA SIFA LAKINI AWATAKAKUONGEZA USAMBAZAJI WA MAJI,AZINYOSHEA VINDOLE TAASISI SISIZOLIPA ANKARA ZA MAJI

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari na watendaji wa Dawasco baada ya kupokea taarifa ya huduma ya maji jijini Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza  katika mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. (wa kwanza kulia) ni
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo (wa kwanza kushoto) akiwa ameambatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja (wa kwanza kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Archard Mutalemwa (katikati) kuelekea katika chumba cha mkutano baada ya kuwasili makao makuu ya Dawasco jana kupokea taarifa ya huduma ya maji jijini Dar es Salaam na Pwani.
waandishi wa habari na watendaji wa Dawasco wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo leo jijini Dar es Salaam.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.




KATIBU mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo amesema kuwa hakuna sababu ya taasisi za Serikali kushindwa kulipa bili ya maji wakati taasisi hizo zinapewa fedha kutokana serikalini na yeye kama katibu aliyepewa dhamana hiyo atahakikisha shirika hilo linaongeza uwezo wa kuhudumia wananchi.
 
Profesa Mkumbo amesema hayo leo katika ziara yake ya kwanza ya kikazi katika shirika hilo, ambapo pamoja na mambo mengine aliipongeza Dawasco kwa kazi kubwa wanayoifanya kwani ukilinganisha na huko nyuma ambapo malalamiko ya maji yamepungua kwa kiasi kikubwa.
Mkumbo amesema haiwezikani mwananchi wa kawaida anamudu kulipa bili ya maji alafu taasisi za serikali ambazo zinapewa fedha zinashindwa kulipa hivyo lazima wahakikishe wanalipa na Dawasco wanatakiwa wafanye kazi hiyo ya kukusanya bili hizo za maji.
 
‘’ Nawapongeza Dawasco kwani mnafanya kazi kubwa binafsi nimekuwa nikiwafuatilia hata kabla sijaingia wizaani kwakweli mnafanya kazi kubwa na mnastahli kupongezwa lakini muendelee hivyo na kwakweli wananchi wanataka maji si vinginevyo.’’ Amesema mkumbo
 
Pia alisema pamoja na kazi kubwa nakudai kuwa watoke kwenye lengo badala yake wahakikishe tatizo la maji linakwisha kabla ya kufika 2020 kwani kuna miradi mikubwa mno ya maji ambayo inatekelezwa na kwakweli kama ikikamilika basi shida ya maji itakuwa limepata suluhisho.
 
Mkumbo ameiongeza kuwa lazima shirika litoke kwenye mtazamo na kuingia kwenye uhalisia n hiyo ndiyo kazi kubwa iliyopo na hapo nikuona watu wanapata maji huku kibainisha maeneo kama Bonyokwa,Pugu,Chanyanyikeni Kinyerezi, maeneo hayo kwa kiasi kikubwa yanakabiliwa na Changamoto kubwa ya maji nay eye kama Katibu amepongeza Dawasco kwa kuliona hilo.
Akiwasilisha wake kwa katibu huyo Ofisa Mtendaji mkuu wa Dawasco Sypriani Luhemeja alisema kuwa shirika hilo limepiga hatua kubwa ukilinganishana na huko nyuma ambapo uzalishaji ulikuwa chini.
 
Amesema hivi sasa Dawasco wanazalisha lita milioni 480 kwa siku na hitaji ni milioni 512 na kudai kuwa kiwango hicho ni kikubwa ukilinganisha na huko nyuma na kwamba bado wamejipanga kikamilifu kuhakikisha kwamba wanamaliza tatizo la maji katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
 
Aidha alifafanua kuwa uzalishaji wa maji katika ruvu chini ni lita milioni 217, ruvu juu lita mil 196 na kutoka mtoni lita 9000 na vyazo vinginevyo vinachangia kwa asilimi ndogo huku akibainisha kuwa jumla ya wateja 187,087 wamehudumiwa na lengo nikuwafikia wateja 400000, ifikapo mwezi juni 2017.
 
Akizungumzia Changamoto Luhemeja alisema ni usambazaji wa maji pamoja na upotevu wa maji ambapo katika kipindi cha mwaka 2015 maji yalipotea kwa asilimia 57 na kufikia mwezi machi mwaka huu maji yamepotea kwa asilimia 37.8.

0 comments: