NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI NA MADINI, DKT. JULIANA PALLANGYO ATEMBELEA MIRADI YA TANESCO KINYEREZI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 3:08 PM
NA
MWANDISHI WETU
NAIBU
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt, Juliana Palangyo, (pichani anayezungumza), ametembelea miradi
ya kuzalisha umeme wa Gesi Asilia ya
upanuzi wa Kinyerezi I pamoja na ule wa Kinyerezi II.
Akizungumza
katika ziara yake ya kukagua miradi hiyo, Dkt Pallangyo ameridhishwa sana na jitihada
zinazofanywa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), katika kuhakikisha Miradi hiyo inakamilika kwa
wakati, ambapo mpaka sasa ujenzi wa mradi wa kinyerezi II umefikia asilimia 53%.
“Niwapongeze
sana TANESCO kwa jitihada kubwa mnazozifanya katika kuhakikisha miradi hii inakamilika
kwa wakati, ambapo mmewezesha Majenereta 8 yenye jumla ya Megawati (MW) 240
mpaka sasa yameshafika, hii ni hatua
nyingine kubwa sana ,hivyo kupitia Mradi
huu wa kinyerezi nina amini Tanzania ya Viwanda inawezekana”.
Akielezea
maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Kinyerezi II, Meneja wa Kituo hicho Mhandisi Steven
Manda alisema kuwa kituo hicho kinaendelea vizuri na ujenzi katika kuhakikisha
kinakamilika Desemba 2018, ambapo mpaka sasa ukamilifui wa Mradi huo unategemea
Kinyerezi I kutokana na Baadhi ya mitambo kuingiliana hasa mitambo ya mfumo wa
upozaji maji ambao utaunganishwa na mtambo wa Kinyerezi I.
Naye
Kaimu meneja wa Kituo cha Kinyerezi I Mhandisi Lucas Busunge amesema kuwa Mradi
huo wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 150, Umeongezewa uwezo wa kuzalisha Megawati
zingine 185 ikiwa ni Awamu ya pili ya upanuzi wa Mradi huo.
Kwa
ujumla miradi yote miwili itakapokamilika, jumla ya Megawati 575MW za umeme
utokanao na Gesi Asilia, zitazalishwa na kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa na
hivyo zitasaidia kuongeza upatikanaji wa Umeme wa Uhakika na kuwezesha wananchi
wengi kupata huduma ya umeme na kufikia
malengo ya Serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda kwa
kuhakikisha Umeme unatumika kama njia moja wapo ya kuleta maendeleo ya wananchi
na kuinua vipato vyao binafsi na Taifa kwa ujumla. Naibu
waziri Pallangyo alifanya ziara hiyo Aprili 20, 2017.
Mafundi wakiendelea
na kazi katika moja ya jengo lilopo katika mradi wa kufua umeme wa gesi asili
megawati 240 wa Kinyerezi I ambapo unafanyiwa upanuzi.
Naibu katibu
Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Pallangyo (wa pili kutoka
kushoto) akiambatana na viongozi wa TANESCO alipotembelea na kukagua maendeleo
ya ujenzi wa Miradi ya Umeme Kinyerezi I&II. Kulia kwake ni kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
TANESCO Bi.Joyce Ngahyoma akifuatiwa na Kaimu Meneja Uhusiano Bw. Yasini Didas
Slayo Kulia pamoja na Meneja Mradi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephen
Manda, (Kushoto)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: