Mwili wa
Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Dk Elly Macha unatarajiwa kuwasili
nchini Aprili 20 mwaka huu ukitokea nchini Uingereza.Dk Macha alifariki
dunia Machi 31 mwaka huu katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton
nchini Uingereza alikokuwa akitibiwa.
Akitoa
ratiba ya msiba huo jana bungeni, Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema
taratibu zote za Uingereza za kurudisha mwili wa Mbunge huo
zimekamilika.“Kule kuna taratibu nyingi za kisheria na kadhalika haikuwa
rahisi kuharakisha mchakato huo, tunashukuru ubalozi wetu wa nchini
humo umeweza kufanikisha jambo hili,”amesema
Ndugai
amesema mwili wake utawasili alhamis ya wiki ijayo katika uwanja wa
Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere April 20, mwaka huu saa
tisa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: