MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA, JAJI FRANCIS MUTUNGI AWATAKA POLISI KUWAKAMATA WALIOFANYA VURUGU MKUTANO WA CUF NA WANAHABARI

 
NA K-VIS BLOG
MSAJILI wa vyama vya siasa amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kulifanyia kazi tukio la watu wanaodaiwa kuwa ni “walinzi” wa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, la kuvamia mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa na kiongozi mmoja wa chama hicho ngazi ya wilaya, na kuwapiga na kuwaumiza watu waliokuwemo kwenye mkutano huo wakiwemo waandishiwa habari.

Naviomba vyombo vya ulinzi an usalama kulifanyia kazi swal hili ili wahusika wafahamike na kuchukuliwa hatua za kisheria. Kwa upande wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inayosimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa, haitasita kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria.” Alisisigtiza.
Mmoja wa watu wanaodaiwa "walinzi" wa Profesa Lipumba, akiwa hoi bin taaban baada ya kupigwa na watu wenye hasira, kufuatia tukio hilo la uvamizi wa mkutano na waandishi wa habari. (Picha ya maktaba)

Jaji Mutungi, amelaani vikali vurugu hizo zilizotokea kwenye mkutano na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, Jumamosi Aprili22, 2017.

“Hivyo, ninalaani vurugu hizo, ambazo zilionekana kuvunja amani na utulivu na watu kuumizwa, tofauti na tunu zetu za taifa za amani na utulivu.” Alisema Jaji Mutungi katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo jijini Dar es Salaam, Aprili 24, 2017.

Alisema amesoma na kuona katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu vurugu hizo zilizotokea katika hoteli ya Vina, Mabibo hapa Dar es salaam, zilizowahusisha watu wanaodaiwa kuwa ni “waklinzi” wa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, ambao walivamia mkutano na waandishi wa habari ulioitishwana kiongozi wa wilaya anayemuunga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

“Ni ukweli usiopingika kuwa, suala la mgogoro wa uongozi katika chama cha CUF lipo mahakamani, lakini nikiwa msimamizi wa Sheria ya Vyama vya Siasa na kutambuliwa na jamii kuwa ni mlezi wa vyama vya siasa; nimelazimika kuwasihi wadau wa siasa hususani wanachama wa chama cha CUF, kutambua kwamba, kuwapo kwa shauri mahakamani siyo fursa ya kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani, kwani jambo hili ni uvunjifu wa sheria na linaleta sura mbaya kwa jamii, alisema Jaji Mutungi katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo Aprili 24, 2017.

Aidha Jaji Mutungi aliwaasa wanachama wa CUF pamoja na tofauti walizonazo, waheshimu utawala wa Sheria.

Alisema Ofisi yake na Jeshi la Polisi vipoo kushughulikia malalamiko yoyote yanayohusu uendeshaji na shughuli za chama chochote cha siasa. Hivyo, hakuna haja ya wanachama wa chama cha CUF kukiuka taratibu za kuendesha chama hicho au kujichukulia Sheria mkononi

0 comments: