KINYEREZI FAMILY YAWAKUMBUKA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA NEW HOPE SIKUKUU YA PASAKA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 1:57 PM
Wadau wa Kinyerezi Family kutowa msaada kwa Watoto
waishio katika mazingira magumu, New Hope kilichopo Tabata, wakisali kwa
pamoja mara baada ya kuwakabidhi Msaada wa vitu mbalimbali, ikiwemo
mchele,nyama,sukari,mayai,nguo na vinginevyo, ili watoto hao nao wapate
kusherehekea vyema sikukuu ya Pasaka
Kinyerezi Family wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watoto wa kituo cha Watoto
waishio katika mazingira magumu cha New Hope kilichopo Tabata,mara baada ya kuwakabidhi msaada wa vitu mbalimbali,ikiwemo
mchele,nyama,sukari,mayai,nguo na vinginevyo,ili na watoto hao wapate
kusherehekea vyema sikukuu ya Pasaka
Pichani
kushoto ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Kinyerezi Family ,Joseph
Manyara na Mdau wakimkabidhi sehemu ya msaada huo Mwanzilishi na Mlezi
wa kituo cha New Hope Organizationi, Bi.Consoler Eliya (katikati). Kituo hicho
kilichopo Tabata,jijini Dar kinalea watoto zaidi ya 150 ambapo kati yao
32 ndio huishi kituoni hapo na wengine huja na kuondoka.
Wana
Kikundi cha Kinyerezi Family wakiwa katika picha ya pamoja na Mama
Mwanzilishi na Mlezi wa kituo cha Watoto waishio katika mazingira
magumu.Consoler Eliya
Mwanzilishi
na Mlezi wa kituo cha New Hope Organization,Consoler Eliya akiwashukuru
wana Kikundi cha Kinyerezi Family kwa kuwakumbuka watu wenye matatizo
mbalimbali kikiwemo kituo chake, kwa kuwapatia msaada wa vitu
mbalimbali,ili na wao waweze kusherehekea kwa furaha siku ya
Pasakam,Concoler amewaomba wana Kikundi hao na wadau wengine mbalimbali
kuwa na moyo wa kujitolea katika suala zima la kusaidia jamii zenye
matatizo,kwani kwa kufanya hivyo hata Mungu huwaongezea zaidi
palipopungua na kuendelea kuwabariki wao na familia zao
Katibu
Msaidizi wa Kikundi cha Kinyerezi Family, Michael Masota akitoa
utambulisho na muongozo mfupi mara baada ya kufika kituoni hapo,kushoto
ni Mwanzilishi na Mlezi wa kituo hicho cha New Hope,Bi.Consoler Eliya
Sehemu ya msaada huo wa vitu mbalimbali
Mmoja
wa wajumbe wa Kikundi cha Kinyerezi Family,Bi Lightness Kweka
akizungumza machache katika hafla hiyo fupi ya kukabidhi msaada wa vitu
mbalimbali katika kituo hicho cha New Hope
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: