IDADI YA VIFO VYA SHAMBULIO LA MABASI SYRIA YAFIKIA 126

Damascus: Karibu watoto wapatao 70 ni miongoni mwa watu waliouawa,kwa mujibu wa idadi ya vifo vya hivi karibuni baada ya gari lililokuwa limetegwa bomu kuyagonga mabasi yaliyobeba abiria waliokuwa wakihamishwa kutoka katika miji iliyozingirwa na serikali nchini Syria. Mlipuko wa Jumamosi iliyopita ulishambulia msafara wa wakaazi wa miji ya eneo la kakazini ya Fuaa na Kafraya, wakati mabasi hayo yaliyokuwa yakipita njia katika eneo linalodhibitiwa na waasi la Rashidin, magharibi mwa Aleppo. Takriban watu 126 waliuawa katika shambulio hilo, kwa mujibu wa Shirika linaloangalia Haki za Binaadamu nchini Syria. Hakuna kundi lililojitokeza kudai kuhusika na shambulio hilo la bomu. Kundi kuu la waasi la Ahrar al-Sham limekana kuhusika na shambulio hilo.

0 comments: