Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (kushoto) akiangalia kabati la nguo katika moja ya chumba cha nyumba za makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Bodi hiyo walizikagua nyumba hizo na kutoa wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi.
Mkuu wa Kitengo cha Majengo wa Idara ya Uhamiaji, Hamza Shabani akiwaonyesha Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, nyumba za makazi za makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga. Wapili kulia ni Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi, watatu kulia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Uhamiaji, Peter Chogero, na kulia ni Mhasibu Mkuu wa Wizara hiyo, Edwin Makene.
Mhandisi wa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg ambayo inajenga nyumba za makazi za Makamishna wa Idara ya Uhamiaji, Leonard Leonidace, akiwafafanulia jambo Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, walipozitembelea nyumba hizo wakikagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba hizo, hata hivyo Wajumbe wa Bodi walitoa wiki kwa Kampuni hiyo kukamilisha ujenzi. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni, Wizara hiyo ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga, na wanne kulia ni Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (Katikati) na Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi (wanne kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi hiyo, mara baada ya wajumbe hao kumaliza ziara yao ya kukagua ujenzi wa nyumba za makazi za Makamishna wa Idara ya Uhamiaji, zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Wajumbe wa Bodi hiyo walitoa wiki tano kwa Kampuni hiyo kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imeipa muda wa wiki tano Kampuni ya Ujenzi ya Koberg Construction Co.Ltd kukamilisha ujenzi wa nyumba za makazi za Makamishna wa Idara ya Uhamiaji hapa nchini zilizoko katika eneo la Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam ambazo zitatumiwa na Makamishna hao.
Uamuzi wa Bodi hiyo umekuja baada ya Kampuni ya Koberg Construction ya nchini hapa kuonyesha kusuasua na kushindwa kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo kwa wakati.
Bodi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga na Katibu wake Bw. David Mwangosi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imefanya maamuzi hayo baada ya kufanya ukaguzi na kujionea hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa nyumba hizo.
Kwa upande wake Katibu wa Bodi hiyo amesema kitendo cha Mkandarasi huyo kusuasua kukamilisha kwa wakati kazi ya ujenzi wa nyumba hizo ulioanza tangu mwaka wa Fedha wa 2014/2015 ndicho kilichoifanya Bodi ya Zabuni ya Wizara hiyo kuamua kutembelea eneo ambalo kazi ya ujenzi wa nyumba hizo unaendelea na kumpatia wiki tano tu kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo.
0 comments: