

Na. Lilian Lundo - MAELEZO
Watanzania wameaswa kutodharau bidhaa zinazotengenezwa ndani ya nchi na kukimbilia bidhaa za nje ya nchi.
Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ameyasema hayo leo, alipotembea
banda la Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO) katika
maonyesho ya viwanda vya Tanzaniaa yanayoendele Uwanja vya Mwalimu J.
K. Nyerere (Saba Saba), Jijini Dar es Salaam.
Dkt.
Mpango amesema kuwa Tanzania haitaweza kuwa nchi ya viwanda ikiwa
watanzania wenyewe hawathamini bidhaa zinazotengenezwa ndani ya nchi.
“Ili
tufanikiwe katika uchumi wa viwanda lazima tuanze kwa kile tunachoweza
kwa kutumia rasilimali tulizonazo ndani ya nchi,” alifanunua Dkt.
Mpango.
Aliendelea
kwa kusema kuwa, watanzania wengi wanadharau mashine ambazo
zinatengenezwa na SIDO ambazo gharama yake ni nafuu ukilinganisha na
mashine zinazotengenezwa nje ya nchi.
Vile vile
amesema kuwa haiwezekani hata jembe la mkono liagizwe toka nje ya nchi
wakati kuna viwanda ndani ya nchi ambavyo vinauwezo wa kutengeneza
majembe yenye ubora.
Aidha
ameishauri SIDO kutengeneza mashine nyingi na kusambaza nchi nzima ili
watanzani waweze kujiajiri na hata kufungua viwanda vidogo vidogo kwa
kutumia mashine hizo.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania (TANTRADE) Edwin Rutageruka amesema kwamba maonyesho hayo
yanafanyika kwa mara ya kwanza na yatakuwa ni endelevu ambapo yatakuwa
yakifanyika kila mwaka mwezi Desemba yakiambatana na maadhimisho ya
Uhuru wa Tanzania Bara.
Ameeleza
kuwa, lengo la monyesho hayo ni kubadilishana uzoefu na kutoa fursa
katika sekta ya viwanda, kutoa hamasa kwa watanzania kununua bidhaa za
ndani ya nchi, kuunganisha wazalishaji na wenye malighafi, kuwawezesha
watafiti na wabunifu kuonana na wenye viwanda, kutoa fursa kwa
watanzania kujua palipo na viwanda pamoja na kuwawezesha vijana na
wanafunzi kujiajiri wenyewe kwa kuanzisha viwanda.(P.T)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: