WAISLAMU WACHANGIA CHUPA 44 ZA DAMU, MADHIMISHO YA MTUME MUHAMAD (S.W.A)
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 2:01 PM
WAISLAMUNA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA
WAISLAMU wa Halmashauri ya Mnispaa ya Kigoma Ujiji Mkoa wa
Kigoma wamechangia chupa 44 za damu ikiwa ni sehemu ya Madhimisho ya Kuzaliwa
kwa Mtume Muhamad ( S.W.A) kila ifikapo
mfungo sita wa mwishoni mwa Mwaka.
Mbali na hilo wamehamasishwa kufanya matukio chanya yatakayoathiri jamii kwa ujumla ambapo
awali walifanya usafi katika makaburi ya yaliyopo kata ya Kipampa kigoma ujiji
kwa nia ya kuimarisha imani,upendo na kulinda amani kwa kuongeza ibada kwa
mwenyezi mungu yatakayosaidia umati wa mtume muhamad iondokane na tamaduni
zisizofaa duniani na akhera siku ya kiyama.
Akifafanua hilo kijiji
cha kidahwe baada ya sherehe hiyo iliyohitimishwa na Mjumbe wa Mashekhe BAKWATA
Shekhe Haruna Kibonajoro ,Katibu wa
Baraza la waislamu mkoani hapa( BAKWATA),Alhaji Shabani Guoguo alisema
madhimisho hayo ni fursa kwa waislamu kubuni mbinu mbalimbali za kutoa sadaka
ikiwemo sadaka kubwa ya damu,ambayo inaokoa mamia ya wahitaji wa damu hiyo
akitolea mfano majeruhi wa ajali na wanawake wanaokabiliwa na uzazi pingamizi.
Alhaji Guoguo alisema ili kuimarisha imani kwa waumini wa
dini hiyo,mashekhe hawana budi kutembea kaya hadi kaya kutoa mawaidha ambayo
yataimarisha imani ya walengwa ili waepukane na janga la ulevi ,uzinifu na
uhalifu wa kutumia silaha za moto sambamba na makundi yanayotumia dini
kudhulumu uhai na mali za watu na kusihi waepuke na migogoro ya kugombea
misikiti.
Jamboleo lilizungumza na Mkuu wa kitengo cha Damu salama
mkoani humo Juma Kiangi juu ya tukio hilo,akiri kupokea makundi ya waislamu
waliojitolea damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wahitaji na walifanikiwa kupata
chupa 44 za damu,ambapo hitaji la mkoa kwa siku ni chupa 1,500 na kutoa wmwito
kwa wadau wengine wakumbuke kutoa sadaka kwa wahitaji ili wapate fadhila kwa mola wao.
Baadhi ya waumini wa dini hiyo Johari Yusuph na Zituni Kabeke
kwa nyakati tofauti wakiri madhimisho ya mazazi ya mtume muhamad (SWA) ni fursa
kwa waislamu kuitumia siku hiyo kwa toba ya dhati kwa kuwa kila aombaye na
kutubu siku hiyo hufutiwa madhambi na hupatiwa kila ahitajilo kwa kuwa ni siku
iliyotakasika kwa mujibu ya kitabu kitukufu cha Q’ruani ambacho kimechakata
utume wake na dhima kwa umati wake.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: