KANAL NDAGALA AKEMEA WATANZANIA WILAYANI KAKONKO- KIGOMA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 1:54 PM
NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA
UCHELEWESHWAJI wa
Malipo ya posho kwa wakimbizi kutoka Nchi jirani imekuwa ni chachu ya kuongeza
kwa matukio ya kihalifu likiwemo la mauwaji kwa nia ya kulipiza kisasi kwa
wananchi wa taifa hili wanaowatumia katika shughuli za kilimo.
Hayo yalisemwa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanal Hosea
Ndagala katika kikao cha dharura cha Balaza la Madiwani
kilichokuwa kikihamasisha shughuli za uhifadhi wa mazingira kutoka shirika
lisilo la kiserikali linalojihusisha na mswala uhifadhi wa mazingira katika makambi
ya wakimbizi hasa Kakonko na Kibondo (Redeso).
Kanali Ndaala alisema baadhi ya
watanzania huwatumikisha wakimbizi mashambani kwa shughuli za kilimo na baadhi yao huwacheleweshea na wengine huwanyima
stahiki zao hali inayosababisha baadhi ya wakimbizi kujihusisha na
vitendo vya uharifu kwa kulipiza visasi hatimaye kutumia silaha za moto kuiba mali na
hata mauwaji.
Baadhi ya washirika wa warsha hiyo ni pamoja na Kasuku Bilago alisema sheria ya
mazingira haina meno hali inayochangia uharibifu mkubwa wa mazingira ,ambapo
wananchi hulima kwenye vyanzo vya maji na kuchoma moto Misitu bila kuchuliwa
hatua za kisheria,ambayo ingewafunza wengine.
Nae Ofisa Mali Asili wa humo Simon
Mando alisema kuwa sheria za mazingira
zipo na zina makatazo yake kinachotakiwa ni viongozi wa ngazi zote kuzisimamia
ili kuepuka madhara makubwa yanaoweza kujitokeza ikiwa hawawajibiki kuelimisha
umuhimu wa utunzaji wa mazingira hali inayokaribisha changamoto ya mabadiliko
ya tabia Nchi.
Baadhi ya Wananchi waliohojiwa na
gazeti hili Filemon Makungu na Masoud
Khalfan walizitaka Mamlaka za Serikali wa vijiji watenge mipango ya matumizi
bora ya ardhi ,ili kuondoa migongano kwa jamii inayochangiwa na viongozi husika ambao wanalima katika vyanzo
vya maji,kujenga makazi ndani ya mita 60 kutoka kwenye chanzo cha maji hali
inayowashawishi raia kuiga .
Akifunga kikao hicho cha siku mbili
Mweneyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Maganga aliwaelekeza Watendaji wa Kata na Madiwani waelimishe
wananchi juu ya uhifadhi wa mazingira na sheria zake kwa kuwa uhifadhi wa mazingira ni pamoja na kuchukua hatua za kisheria kwa
wakaidi wa uhifadhi wa mazingira.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: