Wananchi
wakiangalia daladala lenye namba za usajili T 161 CRP lililoacha njia na
kupinduka Mbagala Misheni kwa Bluda Dar es Salaam leo asubuhi na
kujeruhi watu watatu.
Daladala likiwa mtaroni.
Na Dotto Mwaibale
WATU
watatu wamejeruhiwa vibaya baada ya daladala walikuwa wamepanda kutoka
Temeke kwenda Mbagala Kuu kuacha njia na kupinduka jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na mtandao wa www.habari za jamii.com Dar es Salaam leo asubuhi askari
wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa kipolisi wa Temeke ambaye
hakupenda kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa polisi alisema ajali
hiyo imetokea majira ya saa 12 na nusu asubuhi.
Alisema
daladala hilo liliacha njia na kutumbukia kwenye mtaro eneo la Mbagala
Misheni kwa Bluda baada ya kuteleza kutokana na mvua zilizokuwa
zikinyesha.
Alisema baada ya ajali hiyo wananchi walifika kutoa msaada kwa majeruhi ambao walikimbizwa Hospitali ya Temeke kwa matibabu.
Alitaja
daladala hilo kuwa ni lenye namba za usajili T 161 CRP ambapo alitoa
mwito kwa madereva kuwa waangalifu wanapoendesha magari yao hasa katika
kipindi ambacho mvua zinanyesha.
Jitihada
za kumpata Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi (SACP), Gilles Muroto ili kuzungumzia ajali hiyo
zilishindikana baada ya kupigiwa simu ambayo ilikuwa ikiita pasipo
kupokelewa.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)(P.T)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: