Papa Francis akizungumza na Rais Kabila ndani ya maktaba yake.
Papa Francis akiagana na Rais Kabila baada ya mazungumzo kumalizika.
VATICAN
CITY: Papa Francis amekutana na kufanya mazungumzo ya faragha na Rais
Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mazungumzo hayo
yalifanyika kwenye makazi ya Papa Francis yaliyoko jijini Vatican.
Kwenye
mazungumzo hayo Rais Kabila amesema atahakikisha anafanikisha mazungumzo
ya pande zote zinazokinzana nchini Congo yamalizike kwa amani.
Kwenye
mazungumzo hayo yaliyochukua dakika 20, Papa Francis hakwenda
kusalimiana na mgeni wake huyo kwenye chumba maalum cha wageni maalum na
kumsubiri kwenye maktaba yake.
Vatican
wamesema Papa Francis amesisitiza ni lazima mazungumzo ya amani
yafanyike baina ya serikali na wapinzani ili kuliepusha taifa hilo
kuingia kwenye machafuko.
Na Leonard Msigwa/GPL. (P.T)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: