TRUMP, CLINTON "WAPARURANA" KWENYE MDAHALO WA KWANZA WA KUWANIA KITI CHA RAIS WA MAREKANI



NA K-VIS BLOG/MASHIRIKA YA HABARI
WAGOMBEA wa kiti cha Rais nchini Marekani, Bibi.Hilalary Clinton, wa Chama Cha Democrat, na Bw. Donald Trump wa Chama Cha Republican, “wameparurana” wakati wa mdahalo wa kwanza uliofanyika alfajiri ya leo Septemba 27, 2016  kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu cha Hofstra jijini  New York nchini Marekani.
Katika mdahalo huo wa kwanza ulioongozwa na Lester Holt na uliokuwa live kupitia runinga za nchi hiyo, wagombea hao walitakiwa kujikita kwenye masuala ya Sera ya ya Nje ya Marekani, Usalama wa Taifa hilo kubwa klabisa Duniani, Uchumi, Nishati na Mazingira, Ajira, Ubaguzi na Ugaidi
Wakati Trump, alijinadi kuwa yeye ndiye anayefaa kuliongoza taifa hilo kwa vile anakuja na mkakati mpya wa kulirudishia heshima ya “kimabavu” ya taifa hilo kwani mpinzani wake hawezi kuleta mabadiliko yoyote kwani kwa miaka 30 ya uwepo wa bibi Clinton kwenye anga za kiutawala, hakuweza kufanya lolote.
Naye Bibi Ckinton kwa kejeli alielezea matamshi makali na yenye utata ya Donald Trump, yanaonyesha anavyoishi kwenye uhalisia wa hulka yake, “Donald you live on your reality”.
Hivi ndivyo Donald Trump alivyo “mnanga” Bibi Clinton, walipotakiwa kuelezea mikakati yao katika Sera za Nje na Usalama wa taifa.
“Bibi Clinton, umekuwa ukipambana na wanamgambo wa Kiislamu wa ISIS kwa karibu maisha yako yote ya utu uzima”, Trump alisema.
Naye Bibi Clinton kuhusu suala hilo aliilaumu Russia kwa kuanzisha vita mpya ya kimtandao dhidi ya Marekani na kusema, “Russia na Rais Vladimir V. Putin wameanzisha vita mpya ya kutumia mitandao kwa kufanya udukuzi, wa taarifa nyeti za kibinafsi na za taifa hilo la Marekani kwenye mtandao wa Internet na kwamba, yeye akiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Marekani atahakikisha Russia, China, au kikundi chochote chenye nia mbaya na Marekani, kinadhibitiwa kwa kuimarisha intelijensia na kushirikiana na makampuni yanayoendesha mitandao nchini humo.
Kuhusu suala hilo hilo la Sera ya Nje na Usalama, Donald Trump alisema, “Islamic State(ISIS) wasingeweza kutetemesha ulimwengu kama Marekani ingesalia Iraq, “kuondoka kwa Marekani nchini humo kumeacha mwanya unaowafanya sasa ISIS kufanya watakalo na kutapakaa kote Iraq na Syria, Marekani ilipaswa kuchukua mafuta yote ya Iraq kwani mafuta hayo ndiyo wanayotumia ISIS kujipatia kipato na kuendesha vita na kufadhili washirika wao nje ya Iraq.” Alisema Trump
Trump aliweka msimamo wake kuwa Jumuiya ya NATO haina faida na Marekani, kwani asilimia 70 ya michngo yote ya kuendesha NATO imekuwa ikitolewa na Marekani, na kwamba, washirika wa NATO wameshindwa kuisaidia Marekani kupambana na Ugaidi na badala yake wanafanya mambo yasiyokuwa na faida na Marekani na kwamba yeye akiwa Rais, ni lazima kila taifa litoe mchango sawa vinginevyo Marekani haiwezi kuendelea kuzilinda nchi za NATO bure bure tu, la sivyo watalazimika kulipia gharama.
Hata hivyo Bibi Clintoa alimfahamisha mpinzani wake kuwa Kama ilivyo msimamo wa kisera wa Marekani, aliyeandaa na kusaini makubaliano ya kuyaondosha majeshi ya Marekani nchini Iraq, ni Rais George Bush, na siyo Barack Obama, alichofanya Obama ni kutekeleza maamuzi ya kisera yaliyofanywa na mtangulizi wake kwa niaba ya Marekani, na kuhusu NATO Bibi Clinton alieleza umuhimu wa ushirika huo katika usalama wa Marekani, kwani kila Marekani inaposhiriki vita sehemu fulani ya Dunia, wamekuwa wakishirikiana na wenzao wa NATO katika noperesheni mbalimbali za kijeshi ikiwemo kubadilishana taarifa za kiintelijensia kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi.
Mdahalo wa pili unatarajiwa kufanyika Oktoba 10 na watatu na wa mwisho utafanyika Oktoba 20. Uchaguzi wa Marekani unatarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.









Muongoza mdahalo, Lester Holt

0 comments: