KAMPUNI YA MABIBO BEER YAENDELEA KUDHAMINI TAMASHA LA WAZI LA BURE LA MICHEZO MBALIMBALI JIJINI DAR ES SALAAM
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 10:11 AM
Mmoja
wa waratibu wa tamasha hilo kutoka Kampuni ya Mabibo Beer Wine and
Spirits Ltd, Abdallah Ngoma akizungumza na wanahabari kuhusu bia ya
windhoek na tamasha hilo kwa ujumla.
Mdau wa Windhoek, Kasano Jonathan akizungumzia ubora wa bia ya Windhoek.
Mkufunzi
Mkuu wa Kituo cha mazoezi cha Power on Fitness cha Mwenge jijini Dar es
Salaam Sas Sangandele akizungumzia umuhimu wa kufanya mazoezi.
Wadau wakipata chakula katika tamasha hilo.
Mazoezi yakiendelea.
Hapa sebene na mazoezi kwa kwenda mbele.
Hapa ni mazoezi tu kwa kusonga mbele.
Hapa ni mpango mzima wa midundo ya kamatia chini.
Wadau wa windhoek wakiwa kwenye tamasha hilo.
Hapa ni furaha tu katika tamasha hilo.
Mwonekano wa kivingine wa bia ya Windhoek katika chupa mpya.
Mazoezi yakiwa yamepamba moto.
Na Dotto Mwaibale
WADAU
wa mchezo zaidi 150 wameendelea kunufaika na mazoezi ya bure ya viungo
kutoka kituo cha mazoezi cha Power on Fitness cha Mwenge jijini Dar es
Salaam kwa udhamini wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd.
Akizungumza
Dar es Salaam jana katika tamasha la michezo ya wazi kupitia kituo
hicho, Mkufunzi Mkuu wa Kituo hicho Sas Sangandele alisema mazoezi ni
muhimu sana kwa kila mtu kwani yanajenga afya na kupunguza magonjwa
mwilini.
Alisema
kituo hicho kwa kushirikiana na Kampuni ya Mabibo kupitia kinywaji cha
Windhoek wamekuwa wakifanya mazoezi ya wazi kwa wananchi wote bure
katika viwanja vya Leaders katika wakati unaopangwa.
Alitaja
michezo inayofanyika ni pamoja na mpira wa miguu, kuvuta kamba,
kufukuza kuku na mingineo mingi ambayo inafanyika katika jimu
mbalimbali.
Mmoja
wa waratibu wa tamasha hilo kutoka Kampuni ya Mabibo Beer Wine and
Spirits Ltd, Abdallah Ngoma alisema wanajisikia fahari pale wanaoona
wadau wa bia ya windhoek na wananchi kwa ujumla wanaimarisha afya zao
kwa kufanya mazoezi na baada ya mazoezi wanaburudika na bia ya windhoek
iliyopo sokoni kwa muonekano mpya wa chupa yake huku kinywaji kikiwa
kilekile.
Alisema
kampuni hiyo imedhamini tamasha hilo kupitia kinywaji hicho baada ya
kuona kunamuitikio mkubwa wa wananchi kwa kufanyamazoezi jambo
linalowasaidia wawe na afya bora na kupoza koo kwa bia hiyo ambayo
inakubalika na wengi nchini kutokana na ubora wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: