MAWAZIRI WA JPM "WASHAMBULIA" KAMA NYUKI, NCHEMBA, SIMBACHAWENE, DKT. KIGWANGALA "WAVAMIA" MACHINJIO YAVINGUNGUTI, MKUU WA MNADA WA PUGU AFUTWA KAZI

 Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba, (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Tamisemi, na Utawala Bora), Bw. George Simbachawene, (katikati), na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Khamisi Kigwangala, wakijadiliana jambo wakati 'walipovamia' machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam leo asubuhi Januari 2, 2016. ambapo pamoja na mambo mengine, Mkuu wa Mnada wa mifugo, Pugu jijini Dar es Salaam, amefutwa kazi na maafisa wengine kadhaa kwa "kutafuna" fedha za ushuru wa mifugo


NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

WAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba, amemfuta kazi  Mkuu wa mnada wa pugu na Watumishi waliokuwa zamu tar.24.12.2015 na tar.01.01.2016 na kuagiza wafike kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Jumatatu Januari 4. 2015 kwa maelezo zaidi.
Mbali na kuwafuta kazi watumishi hao Nchemba pia amesitisha kuanzia leo uchukuaji wa Ushuru eneo la mnada wa pugu,badala yake makusanyo yote ya fedha za serikali hizo yatafanyika Machinjio ya Vingunguti kwa kutumia mashine za Elektroniki za EFD,Kwa maana hiyo mnada wa pugu utakuwa unatumika kutoa vibali tu vya mifugo ilikudhibiti ubora wa mifugo inayopaswa kuchinjwa.
Uamuzi mwingine aliouchukua Waziri Nchemba ni
eneo la kuhifadhia nyama lililokuwa limejengwa kwa fedha za Wananchi kushirikiana na serikali lifunguliwe kwaajili ya Wananchi kulitumia kuhifadhia nyama hiyo, awali eneo hilo lilifungwa bila sababu za msingi.Vilevile umeme uliokuwa umekatwa eneo hilo urudishwe hii leo kwaajili ya kuwarahisishia wananchi shughuli zao.
Hatua za kuboresha miundombinu ya Machinjio hayo zimeelekezwa kwa Halmashauri ya Ilala zifanyiwe kazi haraka na kwa ubora.

Hatua hiyo ameichukua leo Jumamosi Januari 2, 2015 ikiwa ni saa chache baada ya “kuvamia” machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam usiku wa manane kuamkia Januari 2.

Baada ya kukuta taarifa za utafunwaji wa fedha za ushuru wa mifugo na malalamiko mengine kibao, Waziri Nchemba aliahidi kuwa asubuhi atarejea tena na kweli  alirejea tena kwenye eneo hilo safari hii akifuatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, na Utawala Bora, George Simbachawene, na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Khamisi Kigwangalla.

Mwigulu alisema, ziara yake ya kushtukiza usiku wa kuamkia leo Januari 2, 2016, iligundua ufisadi wa kukwepa kulipa ushuru wa mifugo ambapo kati ya Ng’ombe 1,450, waliopelekwa kwenye machinjio hayo wakitokea mnada wa Pugu jijini Dar es Salaam, ni 343 tu ndio waliolipiwa na mifugo 1,107 haikulipiwa ushuru, kwa maana hiyo “Wajanja” wametafuna fedha.
Hata hivyo kero za machinjio ya Vingunguti ni nyingi sio kukwepa ushuru tu, bali pia mazingira machafu ya machinjio na ndio maana Mwigulu aliona peke yake changamoto za hapo zitamshinda na kuahidi kurejea tena leo asubuhi.

 






0 comments: