Heri ya mwaka
mpya. Nina furaha kuwafahamisha kuwa kitabu kipya, "Dokta John Pombe
Magufuli: Safari ya Urais, Mafanikio na Changamoto katika Urais wake"
sasa kinapatikana. Kitabu hiki ni mfululizo wa vitabu kadhaa
ninavyotarajia kuvichapisha mwaka huu 2016.
Wakati kitabu
hiki kikiingia sokoni, kitabu kingine kuhusu taaluluma ya Usalama wa
Taifa kipo katika hatua za mwisho, na matarajio ni kukiingiza sokoni
mwishoni mwa mwezi huu.
Kitabu hiki cha
Dokta Magufuli kina sura sita. Katika utangulizi, kitabu kinazungumzia
mazingira ya uchaguzi mkuu uliopita, msisitizo ukiwa kwenye hali ya nchi
ilivyokuwa kabla ya uchaguzi huo.
Kadhalika,
utangulizi huo unaelezea mabadiliko ya ghalfa ya kisiasa, hususan ndani
ya CCM, yaliyojitokeza kufuatia jina la mwanasiasa aliyekuwa maarufu
kuliko wote wakati huo, Edward Lowassa, kukatwa na chama hicho tawala
wakati wa mchakato wa kupata mgombea wake wa kiti cha urais.
Sura ya kwanza
inamtambulisha Dokta Magufuli, kwa kuangalia historia fupi ya maisha
yake. Sura ya pili inaeleza mchakato aliopitia Dkt Magufuli hadi kuibuka
mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM. Sura hii inachambua kwa undani
ushindani miongoni mwa makada zaidi ya 40 waliochukua fomu kuwania urais
kupitia chama hicho.
Sura ya tatu
inaelezea fursa alizokuwa Dokta Magufuli na CCM kwa ujumla katika
kipindi cha kampeni na uchaguzi mzima kwa ujumla. Sura hii inachambua
uimara wa mwanasiasa huyo sambamba na turufu za kawaida za CCM katika
kila uchaguzi. Kwa uapnde mwingine sura hiyo yaangalia pia mapungufu
yaliyopelekea urahisi kwa Dokta Magufuli kumshinda mpinzani wake mkuu
Lowassa, sambamba na mapungufu ya UKAWA yaliyoiwezesha CCM kushinda.
Sura ya nne
inajadili changamoto na vikwazo kwa Dokta Magufuli na CCM kwa ujumla
wakati wa kampeni. Kadhalika, sura hii inazungumzia jinsi Lowassa na
UKAWA walivyoshindwa kutumia changamoto hizo za wapinzani wao.
Sura ya tano
inajadili urais wa Dokta Magufuli tangu aingie Ikulu, wakati sura ya
mwisho inajadili changamoto zinazoukabili urais wake na kutoa
mapendekezo.
Nimejitahidi
kadri nilivyoweza kuandika kitabu hicho kama mtu niliyeufuatilia
uchaguzi huo kwa karibu. Natambua kuna wanaoweza kuwa na hofu kuwa
'niliisapoti CCM na Dokta Magufuli wakati wa kampeni, na kutoiunga mkono
UKAWA na Lowassa.' Naomba kuwatoa hofu kwani kitabu hiki ni si cha
kiitikadi bali kwa ajili ya Watanzania wote bila kujali tofauti zao za
kiitikadi.
UTAKIPATAJE?
Bei ya kitabu
sasa ni Shilingi 4,000 tu. Ili kukipata, nunua kwa M-PESA namba
0744-313-200 jina JOHN ZABLON MPEFO au TIGO-PESA namba 0652-112-071 jina
CHRISTINE JOHN MANONGI
KARIBUNI SANA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments: