Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (wa pili
kushoto) akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Lino International Agency
ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga
(katikati) kushoto Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert
Makoye ( wa pili kulia), Katibu wa Kamati ya Miss Tanzania Bosco
Majaliwa (kulia) pamoja na mpiga picha wa kipindi cha Mimi na Tanzania,
Geofrey Magawa a.k.a KIM (kushoto) wakiwasili Desemba 31, 2015 kwenye
makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge,
Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Miss Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu
amemaliza mwaka 2015 kwa kutembelea kituo Nunge ambacho ni makazi ya
wazee na walemavu wasiojiweza kilichopo Vijibweni, Kigamboni jijini Dar
es Salaam.
Hoyce ambaye amekuwa akisaidia watu wa aina
mbalimbali wenye matatizo ikiwa ni kama moja ya kazi wanazofanya mamiss
kwa jamii pia kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania ambacho
kimekuwa kikisaidia watu mbalimbali na katika halfa hiyo aliongozana na
watu wake wa karibu ikiwepo kamati ya Miss Tanzania.
Katika halfa hiyo iliyodhaminiwa na Malaika
Beach, Hoyce baada ya kuwasili kituoni hapo yeye na timu nzima
aliyoongozana nayo walifanya shughuli za kijamii katika kituo hicho
ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika makazi ya wazee na walemavu
wasiojiweza waliopo kituoni kwa kupulizia dawa za kuulia wadudu katika
nyumba zao, kugawa dawa za mbu, maji, juice na biskuti na baadae
wakapata chakula cha pamoja na wazee na walemavu wasiojiweza.
Akizungumzia halfa hiyo ya kufunga mwaka,
Hoyce Temu alisema kumekuwepo na kusahaulika kwa makundi ya watu
wasiojiweza na jinsi muda unavyokwenda wanazidi kusahaulika na jamii
inayowazunguka.
Alisema yeye kama Miss Tanzania ana wajibu
wa kujitoa kuwasaidia watu wa aina hiyo na amekuwa akifanya maeneo mengi
kwa kujumuika nao kwa kuwapa msaada na kuwafariji kwani nao wana
thamani kama binadamu wengine.
"Kadri inavyokwenda kumalizika karne ya
21 kunazidi kuongezeka kwa makundi ya wasiojiweza na mimi kama Miss
Tanzania nimeamua kujitoa kwa kusaidia makundi haya kwani ni wajibu wetu
na tukumbuke na sisi tunaelekea huko," alisema Hoyce.
Aidha Hoyce alitoa ushauri kwa mamiss
wenzake kuwa wanatakiwa kuisaidia jamii kwa kutumia fursa walizonazo
mbele ya jamii kwa kutoa misaada kwa makundi ya aina mbalimbali.
Alisema kazi ya kusaidia jamii siyo ya
serikali pekee na wao kama mamiss na watu wenye uwezo kwa ujumla wana
wajibu wa kusaidia na sio kutazama mijini pekee kutokana na kundi kubwa
la wasiojiweza kuwa vijijini.
"Sio swala la serikali pekee ...
ukichaguliwa kuwa mrembo unakuwa na malengo ambayo umeyaweka hivyo
watumie umaarufu, sura zao na sauti kufikia watu wa aina mbalimbali
ambao wanahitaji msaada, " Na sio
wazee pekee, 65% ya nchi yetu ni vijana na 20% wanajihusisha na kutumia
madawa ya aina mbalimbali hivyo wanaweza kuwatembelea na kutoa elimu juu
ya athari za utumiaji wa madawa hayo," alisema Hoyce.
Mdau Matukio Chuma na Dada yake Hoyce Temu, Bi. Edith wakifurahi jambo wakati walipowasili kwenye kituo cha Nunge.
Nae Mkurugenzi wa Lino International Agency,
ambayo ndiyo waandaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashimu Lundenga
alimtaja Hoyce kama Miss bora kuwahi kutokea tangu walipoanzisha
shindano la Miss Tanzania mwaka 1994.
Alisema mamiss wengi wamekuwa wakiisaidia
jamii lakini Hoyce amekuwa akijitoa zaidi kuliko wengine na kufanya
shindano hilo kuonekana kuwa na faida mbele ya jamii.
"Naomba niseme ukweli Hoyce anatakiwa
kuwa mfano wa kuigwa haijawahi kutokea miss aliyejitoa kusaidia jamii
kama yeye na wapo wengine wanasaidia ila Hoyce amekuwa mstari wa mbele
kwa hilo tunampongeza na tunamwomba azidi kuwa hivyo," alisema Lundenga.
Kwa upande wa Afisa Mfawidhi wa kituo cha
Nunge, Ojuku Mgedzi amemshukuru Hoyce kwa upendo amekuwa nao kwa kituo
hicho ambacho awali aliwahi kukitembelea 2006 akiwa na marehemu Amina
Chifupa na kumtaka kuzidi kuwa na moyo huo kwa jamii inayomzunguka.
Mgedzi pia alizungumzia changamoto
zinazowakabili kuwa ni pamoja na kutokuwepo kwa uzio hivyo kutokuwa na
hali ya usalama, kuvamiwa kwa eneo hilo na wananchi ambalo lina hekali
50.8 na tayari asilimia 50 imevamiwa na tayari taarifa ipo wizarani na
wanashughulikia na zingine ndogo ndogo Hoyce akiahidi kuwasaidia.
Nae mmoja wa washiriki aliyeongozana na
Hoyce, Tausi Mwenda alisema kuwa amejifunza mambo mengi kupitia halfa
hiyo aliyoifanya Hoyce na kuwashauri watu wa aina mbalimbali kuwa na
moyo wa kujitoa kusaidia jamii kama anavyofanya Hoyce.
Baadhi ya wadau waliombatana na Miss
Tanzania 1999, Hoyce Temu (hayupo pichani) akiwemo Bi. Tausi Mwenda Mke
wa aliyekuwa Meya wa Kinondoni, Yusuph Mwenda, (katikati) wakifurahi
jambo walipowasili kwenye kituo cha Nunge, makazi ya wazee na watu wenye
ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu
akimkumbatia rafiki yake wa siku nyingi mmoja wa wazee wenye ulemavu
uliotokana na ugonjwa wa ukoma, Mganga Shija (66), wakati alipotembelea
makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge,
Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya
shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiendelea
kufurahi na rafiki yake wa siku nyingi mmoja wa wazee wenye ulemavu
uliotokana na ugonjwa wa ukoma, Mganga Shija (66), wakati alipotembelea
makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge,
Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya
shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akitazama
jicho la upande wa kulia linalomsumbua mzee Mganga Shija (66), ambaye
aliomba kusaidiwa matibabu CCBRT wakati alipotembelea makazi ya wazee na
watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es
Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga
mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
Afisa Mfawidhi wa kituo cha Nunge, Ojuku
Mgedzi (kushoto) akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya kituo hicho kwa
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu aliyeambatana na Kamati ya Miss Tanzania
kwenye ziara hiyo.
Mkurugenzi wa Lino International Agency
ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga
akizungumza jambo na Afisa Mfawidhi wa kituo cha Nunge, Ojuku Mgedzi.
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiserebuka na mmoja wa wazee wanaoishi kwenye makazi ya Nunge kituoni hapo.
Bi. Edith (kulia) ambaye ni Dada wa Miss
Tanzania 1999, Hoyce Temu akiteta jambo Bi. Tausi Mwenda mke wa
aliyekuwa Meya wa Kinondoni, Yusuph Mwenda kabla ya kuelekea kwenye
zoezi la upigaji wa dawa.
Baadhi ya nyumbani za makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (katikati)
akiwa na Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa
shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) na Tausi Mwenda
(kushoto) wakichanganya dawa ya kuulia wadudu tayari kwa kupulizwa
katika nyumba kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza
yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Desemba 31, 2015 ikiwa
ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha
mwaka mpya 2016.
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akisaidia
kupuliza dawa ya kuuwa wadudu katika moja ya nyumba kwenye makazi ya
wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni,
jijini Dar es Salaam, Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya
kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akizungumza
na mmoja wa wazee (jina lake halikupatikana) kabla ya kumpigia dawa ya
kuua wadudu nyumbani kwake wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu
wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es
Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga
mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
Dada yake Hoyce Temu, Bi. Edith akishiriki
kuondoa vyakula vyombo ili kuruhusu zoezi la upigaji wa dawa ya kuulia
wadudu kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo
Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni
mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka
mpya 2016.

Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akigawa
chakula kwa watoto katika makazi ya wazee na watu wenye ulemavu
wasiojiweza iliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Desemba 31,
2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na
kukaribisha mwaka mpya 2016
0 comments: