

Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
uzinduzi wa michuano ya Kombe la Shirikisho (AzamHD Federation Cup)
utakaofanyika leo Jumatatu, saa 9 kamili mchana katika uwanja wa Karume
ambapo timu ya Abajalo FC itacheza dhidi ya Transit Camp zote za jijini
Dar es salaam.
Michuano hiyo ilianza kutimua
vumbi jana kwa mchezo mmoja kuchezwa katika uwanja wa Karume uliopo
mjini Musoma, ambapo Vill Squad ya jijini Dar es salaam iliweza kuibuka
na ushindi wa mabao 3- 1 dhidi ya timu ya JKT Rwamkoma ya mkoani Kagera.
Katika uwanja wa CCM Kirumba,
Pamba FC ya jijini humo watakua wenyeji wa timu ya wachimba dhahabu
kutoka mkoani Shinyanga, Bulyanhulu FC mchezo utakaoza saa 10:30 jioni.
Jumla ya timu 64 zinashiriki
michuano hiyo kutoka Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la
Pili kuwania kutwaa ubingwa, ambapo Bingwa wa michuano AzamHD Federation
Cup atapata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho
barani Afrika mwaka 2017.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: