Balozi Sefue pia amesema, Rais ametoa wiki moja na kwa vyovyote si zaidi ya wiki mbili kwa uongozi mpya wa Muhimbili kuhakikisha kuwa mashine zote za uchunguzi wa magonjwa ambazo hazifanyi kazi zinafanya kazi na kuhudumia wananchi kama ipasavyo.
MAGUFULI AVUNJA BODI YA UONGOZI MUHIMBILI ATEUA UONGOZI MPYA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 12:34 PM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli , leo mchana amefanya ziara ya
kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukutana na hali ya
kumsikitisha.
“ Rais amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa
wagonjwa hususan wanaolala chini. Pia amekasirishwa na hali ya
kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi ambapo amekuta
mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa
hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili sasa, ilihali mashine kama hizo
katika Hospitali za binafsi zinafanya kazi na wagonjwa wanaelekezwa
kwenda kutafuta huduma huko”. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
amesema na kutoa maelekezo yafuatayo :
Rais, Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali mmoja wa wagonjwa
waliolazwa kwenye kwenye wodi ya sewahaji, kwenye Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, jijini Dar es salaam leo wakati wa ziara yake ya kushtukiza .
Rais amevunja Bodi ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo
ilishamaliza muda wake na amemteua Prof. Lawrence Mseru , kukaimu nafasi
ya Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili kuanzia kesho tarehe 10 Novemba, 2015.
Dkt. Hussein L. Kidanto ambaye ndiye anayekaimu hivi sasa,
amehamishiwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambako atapangiwa kazi
nyingine.
Balozi Sefue pia amesema, Rais ametoa wiki moja na kwa vyovyote si zaidi ya wiki mbili kwa uongozi mpya wa Muhimbili kuhakikisha kuwa mashine zote za uchunguzi wa magonjwa ambazo hazifanyi kazi zinafanya kazi na kuhudumia wananchi kama ipasavyo.
Balozi Sefue pia amesema, Rais ametoa wiki moja na kwa vyovyote si zaidi ya wiki mbili kwa uongozi mpya wa Muhimbili kuhakikisha kuwa mashine zote za uchunguzi wa magonjwa ambazo hazifanyi kazi zinafanya kazi na kuhudumia wananchi kama ipasavyo.
Tayari Wizara ya Fedha imetoa shilingi bilioni 3 kwa ajili ya
kazi hiyo na kulipa madeni ya ukarabati wa mashine za uchunguzi wa
magonjwa nchini.
Hata hivyo Katibu Mkuu Kiongozi amesema kuanzia sasa hospitali
zote nchini zinatakiwa kutenga fedha kutoka kwenye mapato yao wenyewe na
kuhakikisha mashine na vifaa vyote vya kazi vinafanya kazi wakati wote
(Regular Maintenance).
Balozi Sefue pia metumia nafasi hii kuwaagiza watendaji na
viongozi wote katika sehemu za kazi kuhakikisha wananchi wanahudumiwa
ipasavyo na kazi za umma zinatekelezwa ipasavyo.
“Hakutakuwa na huruma kwa watumishi wa Umma wasiojali wananchi na mahitaji yao” Amesisitiza Balozi Sefue.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
9 Novemba, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments: