MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI SIPHO MAKHABANE KULIPAMBA TAMASHA IA AMANI TANZANIA

Mwenyekiti wa tamasha la kuliombea Taifa Aman pamoja na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, Alex Msama akifafanua jambo wakatio wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 19 kuhusu maandalizi ya tamasha hilo. Kulia ni Mratibu wa tamasha hilo, Hudson Kamoga. (Picha na Francis Dande)
Mratibu wa Tamasha la kuombea amani nchin na uchaguzi mkuu, Hudson Kamoga, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya tamasha hilo, litakalofanyika Oktoba 4 Uwanja wa Taifa jijini. Kushoto ni Mkurugenzi Msama Promotions, Alex Msama. (P.T)
NA MWANDISHI WETU
BAADA ya kumtangaza Mchungaji Solly Mahlangu kutoka Afrika Kusini kuimba kwenye tamasha la kihistoria la kuliombea Taifa la Tanzania Kampuni ya Msama Promotions imemtangaza mwimbaji mwingine wa nchi hiyo, Sipho Makhabane kumsindikiza mwenzake katika tamasha hilo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama amesema kuwa mwimbaji huyo amethibitisha kujumuika na waimbaji kutoka nchi mbalimbali katika tukio hilo muhimu la kuliombea taifa la Tanzania.
Msama alisema kuwa kutokana na ukaribu na uhusiano mzuri kati ya nchi hizi mbili Tanzania iliisaidia nchi hiyo kupata uhuru miaka ya nyuma hivyo wameona wawaalike waimbaji hao mahiri.
Tamasha hilo la kusifu na kuiombea Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu, inatarajia kushirikisha waimbaji kutoka nchi za Zambia, Kenya, Uingereza, Afrika Kusini na Rwanda.
Msama alisema kuwa tamasha hilo linatarajia kufanyika mikoa 10 ambako alifafanua kuwa kutokana na tamasha hilo kutokuwa na wadhamini wameweka viingilio kwa VIP ni Sh. 5000, kawaida Sh. 3000  na watoto Sh.1000.
Mkurugenzi huyo alisema watanzania watambue kuwa baada ya uchaguzi kuna maisha mengine hivyo kutokana na kipindi hiki kigumu Watanzania kuunganisha nguvu ya pamoja na kujitokeza kwenye tamasha hilo ili waiombee nchi yao amani iliyopo iendelee kudumu hata baada ya uchaguzi mkuu kumalizika.
“Maandalizi ya Tamasha la kusifu kuombea nchi amani yanaendelea vizuri, waimbaji wengi watakuwepo kutoka nchi mbalimbali wote kwa pamoja wataimba wimbo mmoja ukiwa ni kwa ajili ya kuiombea nchi yetu amani,” alisema Msama.
Msama aliwataja waimbaji wengine ambao waliothibitisha kuimba katika tamasha hilo ni pamoja na Sarah K  na Solomon Mukubwa (Kenya), Ephraim Sekeleti (Zambia), Ifeanyi Kelechi (Uingereza) huku kwa upande wa Tanzania ni pamoja na Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, John Lisu, Rose Muhando, Christopher  Mwahangila, Bonny Mwaitege, Danny Bulenge, Atosha Kissava na Jesca BM.
Naye mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Hudson Kamoga alitoa wito kwa watanzania kujitokeza huku akisisitiza kuwa uchaguzi unaotarajia kufanyika ni msingi wa kuwaleta pamoja watanzania.
Alisema kuwa kamati imejiandaa vizuri pia kutakuwa na nyimbo za kumsifu Mungu hivyo watanzania watarajie kupata  kilicho bora katika maombezi hayo ya kuliombea taifa.

0 comments: