KESHO NI 'MJENJWA DAY' SIKU YA KUSANYIKO KUU LA WANA UKOO WA MJENJWA KIJIJINI NYEREGETE

Ndugu zangu,
Kesho Jumamosi ni siku ya Kusanyiko Kuu la Wana Ukoo wa Mjengwa Kijijini kwetu Nyeregete, Mbarali, Mbeya. Ni tukio litakalokusanyisha vizazi vyote. Ni shughuli ya kimila na kijamii, hivyo, wote mnakaribishwa.
Kuna ng´ombe atakayetolewa zizini ili atoshe kwa kitoweo kwa wote.
Na asipotosha?
Jibu; Nyeregete kamwe haiishiwi ng'ombe.
Mwenyekiti wenu kesho alfajiri kabisa nitaelekea Nyeregete nikiongozana na makamanda wangu wawili; Manfred na Gustav. Na kanuni za kimila zinabana kweli, maana mwanaukoo hutakiwi kwenda kijijini kwenu kwa asili kwa nauli ya kukopa, nauli uitafute mwenyewe. Uifanyie kazi.
Vinginevyo?
Kwa nauli ya kukopa utakuwa umekwenda kama mtalii tu!
Afrika safari nyingine hazihesabiki kimila.
Goodmorning.
Maggid,
Iringa.

0 comments: