MKUU WA WILAYA YA KINONDONI POUL MAKONDA AZINDUA MPANGO WA KUWAINUA VIJANA WENYE VIPAJI VYA SANAA WA 'KINONDONI TELENT SERCH'
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 4:02 AM
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul
Makonda (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akizindua mpango wa kuwainua vijana
wenye vipaji vya sanaa mbalimbali ujulikanao kama Kinondoni Talent
Search. Kulia ni Mwanamuziki, Peter Msechu na Emanuel Mathias ambaye ni
mchekeshaji maarufu 'MC Pilipili ambao watasaidia kuratibu jinsi ya
kuwatambua vijana hao katika wilaya hiyo.
DC Makonda akiwa amekaa na wanakamati
watakaoshughulikia mpango huo. Kutoka kulia ni mwanamuziki Peter
Msechu, Mchekeshaji maarufu, Emanuel Mathias 'MC Pili pili', Ofisa
Uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Mhowera na Ofisa Utamaduni
wa Wilaya hiyo, Jumanne Mrimi.
Mwanamuziki, Peter Msechu (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni DC Makonda.
Mchekeshaji maarufu, Emanuel Mathias 'MC Pilipili' akizungumza kwenye mkutano huo.
Wanamuziki wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni
Paul Makonda ameandaa mashindano maalum ya wenye vipaji kupata nafasi ya
kutoka kisanii liiitwalo kama 'Kinondoni Talent Search'.
Akizugumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo
asubuhi, Makonda alisema lengo kubwa la kuinua vipaji kwa vijana na
kuwapatia fursa za kimaendeleo kupitia fani zao.
Makonda alisema kuwa 'Kinondoni
Talent Search' ni mpango wenye lengo kuu la kuwatambua vijana waishio
kwenye wilaya ya Kinondoni wenye vipaji vya kuimba, kucheza na
kuchekesha ambao wengi wao wapo katika mazingira magumu kiuchumi.
Makonda alisema mashindano hayo yatawafanya vijana kuepukana na mambo
yanayoweza kuharibu malengo yao ya baadae mfano mzuri ni matumizi ya
dawa za kulevya,ngono zembe na vitendo vya uporaji.
"Ukimiliki kipaji unakuwa unamiliki ajira,ni kujua tu namna ya
kukitumia ili kikufae na kukufikisha utakapo na ndio maana kauli mbiu
ya mpango huu ni kipaji chako ajira yako," alisema Makonda.
Alisema mchakato huo unalenga kuwatengenezea nafasi za mafanikio
vijana wenye vipaji, kuwapatia mafunzo na kuwaunganisha na wadau muhimu
waliopo katika sekta zao, lakini kubwa zaidi ikiwa ni kutoa hamasa kwa
vijana wote wa kinondoni.
Mashindano hayo yatakayosimamiwa na Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni
yamezinduliwa rasmi jana, Mkuu huyo waWilaya akitangaza kamati maalumu
itakayosimamia zoezi hilo, yenye wajumbe watano kutoka ofisi yake pamoja
na baadhi ya wasanii.
Aliwataja wajumbe wa kamati hiyo kuwa ni Jumanne Mrimi ambaye ni
Ofisa Utamaduni wa wilaya hiyo, Sebastian Mhowera Ofisa Uhusiano wa
Manispaa ya Kinondoni huku ikiwahusisha wasanii wa muziki Peter Msechu
,mwanamitindo, Jokate Mwengelo na mchekeshaji maarufu Mc-pilipili.
Makonda alisema Kinondoni Talent Search itachukua takribani mwezi
mmoja na nusu, huku ukijumuisha shughuli za utafutaji vipaji ambapo
utaanzia ngazi ya kata 34 ambapo kutakuwa na mafunzo kwa washiriki,
kuwapa nafasi washiriki kukutana na wadau mbalimbali wanaofanya kazi
kama zao.
Aliongeza kuwa mwisho wa kufunga zoezi hilo kutafanyika tukio kubwa
lenye hadhi ya kimataifa litakalowapa vijana wote nafasi ya kuonesha
vipaji vyao mbele ya mabalozi toka nchi mbalimbali kama sehemu ya
mkakati wa kuwasogeza na wasanii kimataifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: