WILLIUM LUKUVI AKIZUNGUMZA NA WADAU KUHUSU MPANGO WA UENDELEZAJI WA MJI MPYA KIGAMBONI

3
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi akisisitiza jambo wakati wa mkutano na wadau kuhusu mpango wa uendelezaji wa mji mpya wa Kigamboni, Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Meck Sadiki. Sehemu ya wadau hao ni pamoja na viongozi wa taasisi za Serikali, mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s), madhehebu mbalimbali ya dini na taasisi za elimu na ulinzi na huduma mbalimbali zilizopo katika eneo hilo la Kigamboni.
2
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angellah Kairuki akizungumza katika mkutano na wadau kuhusu mpango wa uendelezaji wa mji mpya wa Kigamboni, Dar es Salaam.
4
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Sellasie Mayunga akizungumza jambo wakati wa mkutano huo.
6
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bibi Sophia Mjema akizungumza wakati wa mkutano huo.
5
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi pamoja na Naibu wake Mhe. Angellah Kairuki wakimsikiliza mmoja wa wadau Bw. Nyaronyo Kicheere nje ya ukumbi wa mkutano

0 comments:

RAIS DK. SHEIN, KATIKA UFUNGUZI WA GLOBAL HOSPITAL VUGA MJINI UNGUJA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky  Salim Hassan Turky wakati alipofika kufungua Hospitali ya Global  Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo. (Picha zote na Ikulu) 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia  kufungua Hospitali ya Global  Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky  Salim Hassan Turky 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akipeana mkono wa pongezi na Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky  Salim Hassan Turky baada kuifungua Hospitali ya Global  Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akikata utepekuifungua Hospitali ya Global  Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo (kushoto ni Dkt. K. Ravindranath Daktari Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Hospital (kulia)  Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky  Salim Hassan Turky.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo alipotembelea mashine ya Xray baada ya kuifungua Hospitali ya Global  Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo (wa kwanza kulia) Dkt. K. Ravindranath Daktari Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Hospital. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Daktari Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Hospital Dkt. K. Ravindranath (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky  Salim Hassan Turky wakiangalia mashine ya kufanyia Upasuaji wakati alipotembelea  Hospitali ya Global  Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo baada ya kuifungua rasmi. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akifuatana na Daktari Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Hospital Dkt. K. Ravindranath (kulia), wakati alipotembelea sehemu mbali mbali za kutoa huduma katika  Hospitali ya Global  Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo baada ya kuifungua rasmi. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mwakilishi wa Mwakilishi wa Kampuni ya Global Hospital ya India Dkt. Nagesh Rao (kulia), wakati alipotembelea katika vyumba vya upasuaji vyenye mashine za kisasa baada ya kuifungua Hospitali ya Global  Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo (katikati) Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky  Salim Hassan Turky. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Daktari Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Hospital ya India  Dkt. K. Ravindranath (katikati) wakati alipotembelea chumba cha wagonjwa mahututi (Theatre) baada ya kuifungua Hospitali ya Global  Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo (kulia) Mkurugenzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Dk.Jamala A.Taibu. 
Baadhi ya Madaktar na waalikwa katika sherehe ya ufunguzi wa Hospitali ya Global  Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Hospitali hiyo leo. 
Baadhi ya  waalikwa mbali mbali katika sherehe ya ufunguzi wa Hospitali ya Global  Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Hospitali hiyo leo. 
Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky  Salim Hassan Turky akitoa salamu zake mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)  baada kuifungua Hospitali ya Global  Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo. 
Kaimu Waziri wa Fedha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt. Mwinyihaji Makame Mwadini akisema machache na kumkaribisha mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) kuzungumza na wananchi baada ya kuifungua Hospitali ya Global  Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Global  Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo inayomilikiwa na Kampuni ya Vigor Turky ya hapa Zanzibar ambayo itatoa huduma za Maradhi mbali mbali. 
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na taasisi mbali mbali na waalikwa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Global  Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo inayomilikiwa na Kampuni ya Vigor Turky ya hapa Zanzibar ambayo itatoa huduma za Maradhi mbali mbali.


Na Said Ameir, Zanzibar                                                       
28 Machi, 2015
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza kuwa Zanzibar kama zilivyo nchi nyingine inatambua sekta za Afya na Elimu kuwa ndizo msingi wa maendeleo na ukuaji wa sekta nyingine za kiuchumi na kijamii ndio maana wakati wote imekuwa ikichukuwa hatua mbalimbali za kuziimarisha sekta hizo.
Dk. Shein amesema hayo leo mara baada ya kuzindua rasmi hospitali mpya na ya kisasa ya TASAKHTAA iliyopo Vuga mjini Unguja ambayo imejengwa kwa ushirikiano kati ya kundi la makampuni ya Vigor Turkey Group ya Zanzibar na Global hospitals ya India.
“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua umuhimu wa sekta hizi kwa ustawi wa wananchi wa Zanzibar, ndio maana, tumeelekeza juhudi kubwa katika kuziimarisha kwa kuzifanyia mabadiliko, kutunga sera na sheria madhubuti na kuongeza bajeti ya mwaka kwa sekta hizi kila mwaka” Dk. Shein alisema.
Aliwaeleza viongozi na wageni waliohudhuria hafla hiyo kuwa amefurahishwa na uwekezaji huo wa aina yake katika sekta ya afya na kueleza matumaini yake kuwa hatua hiyo itazidi kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya nchini.
Dk. Shein alisisitiza kuwa azma ya serikali ni kuwa na miradi mingi mikubwa kama hiyo katika sekta zote na kwamba mswada mpya wa sheria uliopitishwa hivi karibuni kuhusu uanzishaji na uendeshaji ushirikiano baina ya Sekta ya Umma na Binafsi ni hatua muhimu katika kufikia azma hiyo.
Alitoa wito kuwepo ushirikiano wa karibu kati ya sekta binafsi na sekta ya umma katika afya na kutolea mfano kuwa hospitali hiyo ya TASAKHTAA kuwa na mashirikiano na hospitali kuu ya Mnazi mmoja.
“hospitali yenu itahitaji msaada mkubwa kutoka hospitali ya Mnazi Mmoja na kinyume chake hivyo mnahitaji kushirikiana”alieleza Dk. Shein na kuongeza kuwa hospitali hizo hazitakuwa washindani.
Katika hotuba yake hiyo alizidi kubainisha kuwa Serikali inaendelea kukamilisha mpango wake wa kuifanya hospitali ya Mnazi Mmoja kuwa ya rufaa ili iweze kutoa huduma nyingi zaidi na bora zaidi kwa wananchi.
Aliongeza kuwa kuimarika kwa huduma za afya nchini kutasaidia kupunguza idadi kubwa ya wagonjwa wanaopelekwa nchi za nje kupata matibabu mara kwa mara.
Dk. Shein ambaye kabla ya kuizindua hospitali hiyo alitembelea vitengo mbalimbali vya hospitali hiyo, alieleza kuvutiwa na vifaa na utalaamu uliopo lakini alisisitiza lugha na mahusiano mazuri kati ya watumishi wa hospitali na wagonjwa.
“Hospitali kama hii inatarajiwa kutoa huduma bora na nzuri, kufanya tafiti, na kuchunguza maradhi pamoja na kuwapa faraja wagonjwa kwa kuwahudumia kwa lugha nzuri” Dk. Shein alieleza.   
Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman alisema Wizara imeupokea mradi huo kwa mikono miwili na kuutaka uongozi wa hospitali kuzingatia sheria na kanuni za uendeshaji wa hospitali zikiwemo za usajili wa watumishi wake katika bodi husika za kitalaamu pamoja na zile zinazohusu madawa.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini kwa niaba ya Waziri wa Fedha alisema sekta ya afya imo katika mpango kabambe wa serikali wa kutoa vivutio maalum vya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji zaidi.
Alibainisha kuwa hadi sasa sekta hiyo iko nyuma katika kuvutia wawekezaji tofauti na sekta nyingine kama ya utalii ambapo nchi inahitaji sana huduma katika sekta ya afya hivyo Serikali itaweka jitihada za makusudi  kuondoa hali hiyo.
“Inawezekana hatujaitangaza sana lakini pia yawezekana ni kutokana na ukosefu wa wataalamu na gharama kubwa za uwekezaji”alisema Dk. Mwinyi na kuongeza kuwa mradi wa TASAKHTAA umeonesha mfano katika uwekezaji katika sekta hiyo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kundi la makampuni ya Vigor Turkey Bwana Salim Turky aliwahakikishia viongozi na wageni waliohudhuria hafla hiyo kuwa uongozi wa hospitali hiyo umedhamiria kutoa huduma bora na na kwa gharama nafuu kwa wananchi wote.
“tutahakikisha wananchi wote wanapata huduma za matibabu na tayari baadhi ya wafanyabiashara wameahidi kusaidia gharama za wananchi ambao hawatakuwa na uwezo kabisa ili wasikose huduma”alibainisha Bwana Turky.
Alisema nia ya hospitali hiyo ni kushirikiana na watoa huduma wengine katika sekta hiyo zikiwemo hospitali za umma hivyo wakati wote.

Alizishukuru mamlaka mbalimbali za serikali kwa ushirikiano wao ambao hatimae hospitali hiyo imeweza kukamilika na kuzinduliwa tayari kuanza kutoka huduma kwa wananchi.

0 comments:

ARSENAL KUMNUNUA WANYAMA NA MITROVIC

Kiungo wa kati wa Southampton Mugubi Wanyama
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anapanga kumnunua kiungo wa kati wa Southampton Mkenya Victor Wanyama na mshambuliaji wa Anderlecht Aleksandr Mitrovic kulingana na gazeti la the Sun nchini Uingereza.
Wenger amejiandaa kutoa kitita cha pauni millioni 30 kwa wachezaji hao wawili,huku Wanyama akigharimu kitita cha pauni millioni 20 naye mshambuliaji huyo wa Anderlecht Mitrovic akigharimu pauni millioni 10.
Inaaminika kuwa Wanyama ataondoka katika kilabu ya Southampton iwapo atachukuliwa na kilabu kikubwa huku naye Mitrovic akiwa amekuwa akifuatiliwa na waajiri wa Arsenal katika kipindi cha wiki chache zilizopotea.
Mitrovic amekuwa akifananishwa na Didier Drogba kutokana na mchezo wake.

0 comments:

MAKAMU WA PILI WA RAIS, BALOZI SEIF IDDI AKIKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO TIMU 60 ZA MPIRA WA MIGUU JIMBONI MWAKE KITOPE.

Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Seti za Jezi na Mipira Mmoja wa Viongozi wa timu 60 zilizomo ndani ya Jimbo la Kitope hapo Kijiji cha Kipandoni Upenja Wilaya ya Kaskazini “B”. Katikati yao ni Mke wake Balozi Seif Mama Asha Suleiman Iddi. 
Baadhi ya vijana wa timu za mitaani zilizomo ndani ya Jimbo la Kitope zilizopata vifaa vya Michezo vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo, Balozi Seif Ali Iddi, wakiwa katika hafla hiyo. 
Kocha na Kepteni wa Timu ya Soka ya Kipandoni Star Jeilan Omar Jeilan akipokea mchango wa shilingi 500,000/- kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya kununulia Posi na Nyafu kwa ajili ya Kwinja chao cha michezo. (Picha zote na – OMPR – ZNZ)

                                     
Na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
28/3/2015.
Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi leo amekabidhi vifaa vya michezo kwa  Timu 60 za Mpira wa soka zilizomo ndani ya Jimbo hilo ili kusaidia nguvu na chachu ya kuimarisha Michezo katika Jimbo la Kitope.

Vifaa hivyo ambavyo ni seti za Jezi na Mipira vyenye Thamani ya shilingi Milioni Nane, Laki Nne na Hamsini Elfu { 8,450,000/- }  vimekabidhiwa kwa timu hizo hapo Kipandoni Wadi ya Upenja Wilaya ya Kaskazini “B”.

Balozi Seif akiambatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wadi ya Upenja na Jimbo la Kitope akikabidhi Seti za Jezi na Mipira kwa Timu za Jimbo hilo zinazoshiriki Ligi ya Kanda ya Unguja,Daraja la Pili na daraja la Tatu.

Na pia akakabidhi mipira kwa 36 ya Mitaani pamoja na timu mbili za watoto wadogo wa  Kijiji cha Kipandoni na kuahidi kuonyesha nia ya kusaidia kuwatengenezea Kiwanja watakachokichaguwa ili kiwe na hadhi ya michezo ya Kitaifa  ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B”.

Akizungumza na Wanamichezo hao Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi  aliwataka Vijana hao kujiepusha na makundi ya baadhi ya watu wanaojaribu kuwashawishi wajiingize katika mambo yaliyo nje ya Sekta ya Michezo.

Balozi Seif alisema ni vyema kwa vijana hao wakaendelea kuwaamini Viongozi waliokubali kuwatumikia katika mambo na harakati zao za kila siku hasa zile za michezo ambazo kwa sasa husaidia kutoa ajira.

Aliwataka wanamichezo hao kupitia Viongozi wao waangalie utaratibu wa kutafuta kiwanja kitakachowekewa miundo mbinu ambayo baadaye kitakidhi mahitaji ya kuchezewa Ligi yenye hadhi ya Kitaifa.

Mapema Mke wa Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi alisema katika kuunga mkono juhudi za wanamichezo hao alisema ni vyema kwa wanasoka hao wanzishe utaratibu wa kuanza kuchangia hata kwa kiwango kidogo ili kuwapa nguvu Viongozi na wafadhili wanaoonyesha nia ya kuwasaidia.

Mama Asha alisema Viongozi wa Jimbo hilo watashawishika na kuongeza nguvu zao kwa Timu ambazo  tayari zimeshajikubalisha kujisaidia zenyewe zikisubiri nguvu za ziada.
Mapema Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar Wilaya ya Kaskazini “ B” Tongoa Moh’d Hassan alisema Wilaya hiyo bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa Kiwanja cha soka chenye hadhi inayokubalika kwa michezo mikubwa.

0 comments:

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA VIONGOZI WA KAMATI YA AMANI MKOA WA DAR ES SALAAM

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa Viongozi wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akiwahutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Viongozi wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam leo. (Picha zote na Freddy Maro)

0 comments:

ZITTO KABWE AZINDUA CHAMA CHA ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARECY(ACT) DAR ES SALAAM LEO

 Mwenyekiti wa Chama cha  Alliance for change and Transparecy (ACT)  Anaa Elisha    Akiwashukuru wanachama wote walioshiriki walio kiunga Mkono chama hicho nawaliotoka vyama vingine wakiwemo viongozi na Taasisi Mbalimbali.
 Mwenyekiti wa Chama cha  Alliance for change and Transparecy (ACT)  Anaa Elisha, akiwasalimia wanachama kwa Salam ya chama hicho 

Kiongizi MKuu wa chama  hicho na akiliyekua Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zitto Kabwe. akizungumza na wanachama Mbalimbali toka Nje na Ndani ya Dar es Salaa  katika uzinduzi wa chama hicho na kuwaomba wanachama popote walipo waipigie  Kura ya Hapana  Katiba Pendekezwa.
Kikundi cha Ngoma ya Asili ya Kutoka Kigoma kwa jina maarufu kwa Mkoa huo wa kigoma inaitwa Usambere ikitoa burudani katika uzinduzi huo
Wanachama wa chama hicho kwa makundi mbalimbali wakiingia katika ukumbi kwa nyakati tofauti
Wafuasi wa Chama hicho wakiwa na mabango wakiingia Ukumbini

Wafuasi wa Chama hicho wakiwa na mabango yenye Ujumbe tofauti wakiingia Ukumbini

Wafuasi wa Chama hicho wakiwa na mabango yenye Ujumbe tofauti wakiingia Ukumbini
Wanakikundi wa kasimbo Asili, toka Mkoa wa Kigoma Kijiji cha Nyarubanda Kataa ya Mkigo Wilaya ya Kigoma wakitoa salam ya Chama hicho wakiwa wanajiandaa kuingia kwa Nyimbo za Ali ya Mkoa wao katika Mkutano wa Uzinduzi wa Mkutano wa  Alliance for change and Transparecy (ACT)
Baadhi ya Wafuasi wa Chama hicho wakiingia Ukumbini
Msanii Afande Sele akiwa na wanachama wa Alliance for change and Transparecy (ACT) katika Picha ya pamoja kwenye Uzinduzi wa Chama hicho
Baadhi ya wajumbe na Viongozi wa Chama hicho wakimsikiliza Zitto Kabwe alipo kua akizindua Mkutano wa Chama hicho(wa tatu kushoto) ni Baba wa  Kiongizi MKuu wa chama  hicho na akiliyekua Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zitto Kabwe.,

Msanii  wa Makomando Said Christopher akisalimia Viongozi alipopanda juukwaani na mwenzake

 Mwenyekiti wa Chama cha  Alliance for change and Transparecy (ACT)  Anaa Elisha akisalimiana na
Kiongizi MKuu wa chama  hicho na akiliyekua Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zitto Kabwe mara alipo maliza kuzungumza na wafuasi wa chama hicho

 Mwenyekiti wa Chama cha  Alliance for change and Transparecy (ACT)  Anaa Elisha akisalimiana na Askofu Mstaafu wa Jimbo la Kigoma Angilikana Gerald Mpango  baada ya kuzungumza na Wanachama
Afande Sele akiwa Jukwaani akitumbuiza
Wasanii wa Kikundi cha Makomando wakitoa Burudani, kulia ni fred felix na Said Christopher
Wafuasi wa chama hicho wakijiandikisha na kupatakadi ya Uanacha
Wanachama
Mamia wajitokeza Uzinduzi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Zitto Kabwe akisoma Fomu ya Chama hicho inayomtaka kila mwanacha Ngazi ya juu atangaze Mali zake
Kasimbo Asilia ikitoa Burudani katika Mkutano wa chama cha Alliance for change and Transparecy (ACT)  katika Ukumbi wa Diamondi Jubilee Dar es Sallam leo mara baada ya chama hicho kufanya Uzinduzi 
  Kasimbo Asili ni Kikundi cha Usambere  kutoka Mkoa wa Kigoma katika kijiji cha Nyarubanda Kataa ya Mkigo Wilaya ya Kigoma ikitoa burudani, pichani ukiona wakiruka na kupokezana kwa katika kucheza. 
Wanachama Mbalimbali wakifatilia kwa makini katika Mkutano wa Uzinduzi wa chama hicho Dar es Salaam leo katika Ukumbi wa Alliance for change and Transparecy (ACT)
Vikundi mbalimbali Vikitoa maigizo katika Uzinduzi wa Chama hicho
Wanachama wakijipanga wakati Viongozi wa Chama hicho Kitaifa wakitarajia kuingia katika Ukumbi wa  Diamondi Jubilee
Wanachama wakijipanga mikono wakati Viongozi wa Chama hicho Kitaifa wakitarajia kuingia katika Ukumbi wa  Diamondi Jubilee na baadhi ya wanachama wakipunga mikono kwa kuonyesha alama ya chama chao
 (kulia) akiwapungia mikono wanachama alipokua akiingia katika Ukumbi wa Diamondi Jubilee Dar es Sallam leo (kushoto) ni  Kiongizi MKuu wa chama  hicho na akiliyekua Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zitto Kabwe.

Ulipoimbwa wimbo wa Mungu Ibariki.
Wanachama wakiimba Wimbo wa Taifa
.Katibu Mkuu ACT Tanzania Samson Mwigamba akizungumza na wanachama alipokua akifafanua jambo  (PICHA NA KHAMISI MUSSA)

0 comments: