CHRISTIAN BELLA 'KING OF THE BEST MELODIES' AAHIDI MAKUBWA SHOO YA VALENTINE'S DAY, DAR LIVE
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 10:01 PM
PREZIDAA
wa Bendi ya Malaika Music, Christian Bella 'King of the Best Melodies'
amewaahidi shoo kali mashabiki wake watakaohudhuria katika Ukumbi wa
Kisasa wa Dar Live, Jumamosi ijayo ambayo ni Siku ya Wapendanao
'Valentine's Day'. Staa huyo ameyasema hayo hivi punde wakati wa mkutano
na wanahabari wa vyombo mbalimbali uliofanyika katika ofisi za Global
Publishers.
Bella
amesema atakuwepo ndani ya kiwanja hicho mapema kuanzia saa 7 mchana na
atapiga picha za red carpet na mashabiki wake watakaohudhuria sambamba
na kuzungumza nao mawili-matatu. Mbali na kuwahi ukumbini, Bella
amewaandalia nyimbo zake zote kali za mapenzi kama vile Msaliti, Safari
Siyo Kifo, Nakuhitaji pamoja na wimbo bora uliofunga mwaka wa Nani Kama
Mama.
Kuonyesha
kuwa utakuwa Usiku wa Wapendanao, Bella amewaandalia mashabiki wake
zawadi ya wimbo mpya uitwao NASHINDWA ambao atauchia kwa mara ya kwanza
huku video akienda kuifanyia nchini Afrika Kusini wiki ijayo. Mbali na
Bella usiku huo ambao ni maalum kwa wapendanao, mkali wa muziki wa
Mwambao, Mfalme Mzee Yusuf naye atakuwepo katika kuwaburudisha mashabiki
wote watakaokuwepo ukumbini hapo.
Usiku
huo Mzee Yusuf atashuka na kundi lake la Jahazi Modern Taarab na
kuangusha ngoma zake zote kali za mapenzi kama vile My Valentine,
Wapendanao, Tiba ya Mapenzi, Wasiwasi Wako pamoja na hii ambayo ni
habari ya mjini kwa sasa ya Mahaba Niue.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: