Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
3:08 PM
RB
namba WH/RB/6335/2014-SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI kwenye Kituo cha
Polisi cha Wazo Hill, Tegeta jijini Dar, imemtia mbaroni mtangazaji
maarufu Bongo aitwaye Hanifa Hamidu ‘Lady Hanifa’ na mwenzake aliyetajwa
kwa jina moja la Aneth kwa madai ya kutaka kumuua mhudumu wa baa
aliyetambulika kwa jina la Aika Andrew (32).
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba sakata hilo la kusikitisha
lilijiri wiki iliyopita kwenye baa maarufu ya Shayo iliyopo Tegeta, Dar.
Maelezo yaliyoandikishwa na Aika polisi yalidai kwamba Lady Hanifa
alifika kwenye baa hiyo ambayo ndani yake anamiliki jiko la chakula na
kuelezwa kwamba, siku moja kabla ya tukio hilo alikuwa na deni na
alipofika tu, Aika alimkumbushia ndipo balaa lilipoanza.
Kwa mujibu wa mashuhuda, katika tukio hilo lililojiri mishale ya saa
11:00 jioni, Hanifa alipofika aliingia moja kwa moja jikoni kuangalia
biashara yake kisha akarudi kukaa sehemu ya baa.
Ilisemekana kwamba Aika alimfuata na kumwambia kuwa jana yake alikuwa
akidaiwa bia moja tu ya baridi aliyokuwa amekopa, kitendo
kilichompandisha hasira na kuona kama amefedheheshwa kudaiwa mbele za
watu.
Ilidaiwa kwamba alimwita mfanyakazi wake, Aneth ili ampatie fedha
aliyokuwa akidai Aika lakini muda huohuo Lady Hanifa akaanza kudai
chenji yake kwa mabavu.
Ilidaiwa kwamba kulitokea majibizano makubwa ndipo mtangazaji huyo akaanza kumshambulia Aika huku akipewa sapoti na Aneth.
Iliendelea kudaiwa kwamba katika purukushani hizo, Aneth aliyekuwa
ameshika kisu alimchoma nacho Aika tumboni, kichwani, mikononi huku Lady
Hanifa akimuunguza shingoni kwa kutumia upawa wa chipsi uliokuwa na
mafuta ya moto kisha wakakimbia.
Habari zilieleza kwamba baada ya hapo Hanifa na Aneth walikimbilia
Kituo cha Wazo Hill kutoa taarifa lakini muda mfupi wasamaria wema
walifika katika kituo hicho wakiwa na Aika aliyekuwa ametapakaa damu
mwili mzima.
Polisi waliwashikilia Lady Hanifa na Aneth na Aika akakimbizwa Hospitali ya Mwananyamala.
CREDITS:GPL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments: